Je, bibi na babu wanahitaji mazoezi? 

Mara nyingi huwa tunawaambia wazee wenye umri zaidi ya miaka 65 wapumzike nyumbani. Na kupumzika huku hatutaki wajishughulishe na kazi ndogondogo. 

Lakini wazee wanahitaji mazoezi ya viungo kama watu wengine.  Mazoezi haya yanasaidia katika kuimarisha mifumo mbalimbali katika miili yao kama mfumo wa upumuaji na mzunguko wa damu.

Pia mazoezi humkinga mzee na magonjwa ya kusahau na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kama shinikizo la damu na kisukari

Mazoezi gani yanafaa kwa wazee?

1: Mazoezi ya kusaidia mfumo wa upumuaji na mzunguko wa damu

Mazoezi kama kutembea kuendesha baiskeli na kuogelea husaidia katika kuimarisha mfumo wa upumuaji na mzunguko wa damu.

2: Mazoezi ya kutumia nguvu pia yanahitajika ili kuimarisha misuli. Haya mazoezi Hufanyw mtu akiwa amelala chini na kujaribu kukaa bila ku kunyanyua miguu (sit ups).Hii huimarisha misuli na kukufanya uwe mwenye nguvu

3:Mazoezi ya kujinyoosha kama Yoga husaidia katika kutunza kumbukumbu na kusaidia ubongo kufanya kazi vizuri zaidi.

 

Kama umekatazwa na daktari kufanya mazoezi kwa ajili ya hali yako tafadhali zingatia. Ni vizuri kabla ya kufanya mazoezi ya nguvu nyingi umuulize daktari kama unaruhusiwa kufanya mazoezi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show