Kuogelea ni zaidi ya kukimbia na kunyanyua vyuma

Kuogelea ni starehe na pia ni sehemu ya mazoezi , tena ukiogelea ni kama umefanya mazoezi zaidi ya aina mbili. Ingawa haijawa tamaduni  ya waafrika wengi hasa watanzania kuogelea na hata kwa wengine kuonekana ni sehemu ya michezo kwa watoto wadogo.

Unapoogelea  unaufanyisha mwili mzima mazoezi yaani mikono,miguu na kiwiliwili chote na hapa ndipo unapokuwa umefanya mazoezi ya aina nyingi. Ikiwemo ya aerobics(cardio), anaerobics kama kunyanyua uzito au kuvuta uzito na hata mazoezi ya kulainisha na kunyoosha viungo.

Kuogelea kama zoezi husaidia katika vitu vifuatavyo;

a) hukufanya kuwa mwepesi yaani maji  hukubeba pale unapoogelea na wala mtu hatumii nguvu anapoogelea japokuwa anatumia misuli yote ya mwili na kuifanya laini

b) husaidia kudhibiti matatizo ya viungo hasa jointi ; kusukuma maji unapoogelea hulinda maungio hayo ya viungo na si kama pale mtu akiwa ana matatizo ya maungio na kushindwa kukimbia

c) huongeza nguvu ya misuli yako kwa kuiongezea nguvu.

d) hupunguza msongo wa mawazo na kukupa mapumziko hata baada ya kazi na shughuli tofauti

e)huufanyisha ubongo mazoezi pale ambapo unatumia akili katika kuogolea kwa staili tofauti ikiwemo kulea na nyingine nyingi

f)kwa watu wenye ngozi kavu kuogelea yaweza kuwa tiba ya ngozi kwasababu itapata maji mara kwa mara na hivyo kulainisha ngozi.

Sasa, ni wakati gani inafaa zaidi kuogelea? Muda wowote ule katika siku ni sahihi kabisa ,ila inashauriwa zaidi masaa ya jioni. Hii ni kwasababu ni katika muda huu joto la misuli haliwezi badilika sana kutegemea joto la nje na hapo misuli huweza kustahimili zoezi kwa utumikaji wa nguvu iliyopo kwenye misuli.

Kuogelea mida ya jioni inashauriwa zaidi kwasababu mtu hatokuwa na mawazo ya shughuli anazopaswa kufanya kama inavyokuwa asubuhi na badala yake husaidia kuondoa  uchovu baada ya kazi za siku nzima na kumpa pumziko sahihi

Ikiwa kuogelea ni sawa na kuwa umefanya mazoezi zaidi ya aina tatu hivyo basi ni vyema kama ukiwa na ratiba ya kuogelea walau mara moja kwa wiki iwezekanapo. Hata utajenga mwili,utapata afya nzuri ya mfumo wa upumuaji na mfumo wa damu na pia utasaidia misuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show