MAZOEZI: Pande Mbili za Sarafu

Mazoezi ya kiungo kimoja au baadhi, wakati viungo vingine vimeachwa bila kazi ya kufanya, si salama. Ni sawa na kufanya ukarabati wa tairi moja la gari na kutegemea litakuwa na uwezo wa kusukuma gari zima…

Kama msuli mmoja tu au baadhi ndio hufanyiwa mazoezi, sehemu hii tu ndio itakayoimarika na kukua, hivyo kupelekea kuharibu uwiano wa ukuaji wa mwili kwa ujumla. Hili linaweza lisiwe dhahiri katika muonekano wa nje, lakini ni hakika kuwa lipo na madhara yake yaweza kuanza kuonekana muda mrefu sana baadae. Mchanganyiko wa mazoezi mbalimbali utapelekea kutumika kwa viungo na misuli yote ya mwili, kama ipasavyo.

Vivyo hivyo, si vizuri kuacha kufanyia mazoezi viungo fulani, kwa sababu tu ya maumivu wakati wa mazoezi. Maumivu haya yanatokana na asili ya mwili wenyewe inayotoa nguvu na uhai kwa viungo hivyo ambavyo vimekufa kiasi kwa kutotumika. Mazoezi ya viungo hivi vilivyolala yataleta maumivu kiasi, kwa kuwa asili ya mwili inaviamsha kwenda kwenye uhai.

Mazoezi ya aina yeyote kama ambavyo utaona vyema kwako, hutakiwa kufanyika kwa mpango, na hasa kwa viungo vilivyoachwa muda mrefu bila kazi, ili viweze kuimarika kwa kutumika.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show