Ni kiu tu hauumwi

Mwanasayansi mmoja alisema, ‘Wewe sio tu unachokula, ni unachokunywa pia”. Maji yanakadiriwa kuwa asilia 60-70 ya miili yetu. Maji haya ni kama bahari ,ambapo bahari moja ni ile izungukayo seli na nyingine ni iliyopo ndani ya seli ya mwili.

Maji kama yalivyo na nafasi kubwa katika mwili vivyo hivyo husaidia katika shughuli tofauti za mwili ikiwemo kuupoza mwili na nyingine nyingi na hii ni kwasababu yapo katika seli zote za mwili.
Ukosefu wa maji mwilini,humsababisha mtu kuwa na dalili za kuumwa. Hivyo,si mara zote tunaumwa mara nyingine hatuna maji ya kutosha mwilini na hivyo kujisikia na dalili zote za kuumwa.
Tuone basi maji hufanya nini mpaka tuyakosapo tunajisikia wagonjwa;
a)hufanya mwili kuwa na nguvu na kuondoa uchovu,na hivyo kuongeza muamko zaidi wa akili yako.
b)huondoa sumu mwilini, kwa kukojoa na kutoa jasho na kwa hili kupunguza hatari ya UTI na mawe kwenye figo na magonjwa mengine yanayohusiana na hayo.
c)huimarisha kinga ya mwili
d)maji ni dawa pale unapoumwa kichwa,kwakuwa hali hii kwa mara nyingi hutokea pale mwili usipokuwa na maji ya kutosha. Hapa ndipo ule msemo heshimu kiu yako kwa kuwa ina sababu ya kuwepo unapokuja.
e)huzuia kuumwa kwa maungio ya viungo na misuli kwa kuwa maji ni kilainishi.
f)huboresha mng’aro wa ngozi na kuzuia mikunjo na pia kuzuia harufu ya jasho
g)maji pia husaidia mmeng’enyo wa chakula na kuepusha magonjwa kama kiungulia na tumbo kujaa gesi.

Usinywe dawa ,kunywa maji badala yake sio kila kuumwa kunahitaji dawa.

2 thoughts on “Ni kiu tu hauumwi

    1. Asanteee sana,tunafurahi unapojifunza na tunashukuru kwa kutembelea tovuti yetu. Endelea kuwafahamisha wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show