KIUNGULIA WAKATI WA UJAUZITO .

 

Ujauzito ni habari njema na ni safari ya miezi 9 yenye kuleta furaha. Vipo vitu mbalimbali vinavyoweza kuingilia furaha ya mimba vikiwemo kiungulia. Kiungulia hutokea mara nyingi  kuanzia wiki ya kumi na tatu na kuendelea ingawa kwa wengine hutokea mapema zaidi.

Kiungulia wakati wa ujauzito si dalili ya hatari na hutokana na sababu kadhaa zikiwemo:

Kondo la uzazi kuzalisha kichochezi(homoni) kiitwacho progesterone ambacho hutunza mimba. Kichochezi hiki husababisha misuli midogo inayotengeneza utenganisho kati ya Koo la chakula na tumbo kulegea (relax) . Hii husababisha njia hii isifunge kabisa hivyo kupelekea mchanganyiko wa chakula na tindikali tumboni kurudi katika Koo la chakula hivyo kuleta kiungulia.

Pia ukuaji wa mtoto husababisha mgandamizo katika mfumo wa chakula kusababisha chakula kilichochanganyika na tindikali kurudi katika Koo la chakula.

Zipo njia mbalimbali ambazo mama huweza kutumia kupunguza Hali hii ikiwemo

  • Kupunguza au kuepuka vyakula au vinywaji vyenye gesi na machungwa
  • Epuka au punguza kula vyakula vyenye viungo vingi kama pilau.
  • Kula chakula kwa kiasi kidogo mara nyingi huweza kupunguza uwezekano wa kupata kiungulia.
  • Kuepuka Kula muda mchache kabla ya kulala,ambapo inashauriwa ule masaa mawili au matatu kabla ya kulala.
  • Unashauriwa kutumia mto wakati wa kulala.
  • Epuka mavazi ya kubana wakati wa ujauzito.

Furahia kipindi cha ujauzito kwa kuepuka karaha mbalimbali kama hizi,tatizo linapozidi pata ushauri wa daktari.

 

Reviewed by Dr. Msiry

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show