HEDHI: Viashiria sita (6) vya kumuona Daktari

Ni kawaida kwa mwanamke kuona siku zake kila mwezi. Lakini je, utajuaje kama hedhi anazopata mwanamke ni kawaida au kuna tatizo?

Kwa kawaida, hedhi huchukua wastani wa siku 2 hadi 7. Mzunguko wa hedhi kwa wastani ni wa siku 28, ingawa pia ni kawaida kuwa na siku kadhaa pungufu au zaidi.

Baadhi ya mabadiliko ya hedhi yanayoweza kuashiria kuwa kuna tatizo ni yafuatayo :

  1. Kutokuona siku zako / Kuruka mzunguko wa mwezi

Mara nyingi hii hutokea kama mwanamke amepata ujauzito. Kama umekuwa na mahusiano ya karibu na mwenzi wako katika kipindi cha karibu, waweza kupima mkojo kuona kama una ujauzito. Pia, fika katika kituo cha afya kwa ajili ya vipimo zaidi.

Aidha, hii inaweza pia kusababishwa na msongo wa mawazo, kupungua uzito kwa ghafla, unene uliopitiliza, kufanya mazoezi kupita kiasi, utumizi wa vidonge vya uzazi wa mpango, umri zaidi ya miaka 49, na baadhi ya magonjwa katika mfumo wa uzazi.

  1. Kutokwa na damu kabla ya siku zako / baada ya tendo la ndoa

Hii yaweza kutokana na maambukizi ya vijidudu, matatizo ndani ya mfumo wa uzazi au saratani. Pia kwa watumiaji wa tiba ya vichocheo katika miezi 3 ya Kwanzaa

  1. Kutokwa na damu nyingi au kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida

Hii yaweza kusababishwa na saratani ya mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi au mabadiliko yanayotangulia saratani.

  1. Kuona siku zako baada ya kutimiza umri wa kuacha (menopause)

Si kawaida kwa mwanamke aliyetimiza umri, kuendelea kutokwa na damu zaidi ya miezi 12 baada ya kuacha kuona siku zake. Yaweza kuwa kwa sababu ya saratani ya mfuko wa uzazi, mlango wa mfuko wa uzazi (cervix), saratani katika uke (vagina) n.k.

  1. Kutokwa na uchafu wakati wa hedhi

Uchafu huu unaweza ukawa unatoa harufu, wa rangi ya kijani au umechanganyika na damu. Hii yaweza kuashiria uwepo wa maambukizi.

6. Maumivu makali sana (yasiyo ya kawaida) wakati wa hedhi

Yaweza kusababishwa na uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids), seli za mfuko wa uzazi kuota nje ya mfuko wa uzazi (endometriosis) pamoja na magonjwa mengine. Pia, yaweza kutokuwa na sababu yeyote dhahiri.

Hedhi yaweza kubadilika. Mabadiliko haya sio mara zote humaanisha kuna tatizo, lakini ni muhimu kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi ili kuwa salama.

2 thoughts on “HEDHI: Viashiria sita (6) vya kumuona Daktari

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show