Je, unafahamu kuhusu maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke?( PID)?

Mmoja kati ya wanawake nane waliowahi kuugua PID hupata shida kupata ujauzito

PID ni nini?

PID ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika njia ya uzazi wa mwanamke ambao huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS),nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)

Nani yupo katika hatari ya kupata PID?
Upo kwenye hatari ya kupata PID kama:-
•Umewahi kupata ugonjwa wa zinaa na haukutibiwa (kama klamidia).
•Unajamiiana na mtu zaidi ya mmoja.
•Mpenzi wako ana wapenzi wengine zaidi yako.
•Una historia ya kuugua PID.
•Una umri wa miaka 25 au chini na umeanza kujamiana.
•Unatumia kitanzi kama njia ya uzazi wa mpango hasa wiki tatu za kwanza.

Dalili za PID ni zipi?
•Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
•Homa.
•Kutokwa na ute ukeni wenye harufu kali.
•Maumivu na/au kutokwa na damu wakati wa kujamiiana
•Mkojo kuunguza wakati wa kutoa haja ndogo.
•Kutoka damu kabla au katikati ya mzunguko wako wa hedhi.
•Maumivu ya mgongo kwa chini karibu na kiuno.
Hata hivyo, unaweza usijue kama una PID kutokana na kuwa na dalili chache au kutokuwa na dalili kabisa. Hivyo ni kuna haja ya kujiepusha na vihatarishi vya ugonjwa huu kwa:-
•Kuepuka kufanya ngono isiyo salama.
•Kuwa na tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa vipimo vya uzazi.
•Kutokufanya mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi imefunga vyema.
•Kuwa msafi na kula lishe bora.

Nini athari za kutokutibiwa PID mapema?
•Kupoteza uwezo wa kushika mimba.
•Mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi.
•Maumivu ya tumbo na kiuno ya muda mrefu.
•Kuziba kwa mirija ya mfumo wa uzazi.

Kama PID itagundulika mapema inatibika hivyo ni vyema kumtembelea daktari pale tu uonapo dalili za ugonjwa huu.
HAKIKISHA, unamwambia mwenza wako ili nae aweze kupimwa na kutibiwa magonjwa ya zinaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center