Jino langu limetoka, nitapata Jino bandia leo leo?

Ulishawahi kujiuliza itakuwa vipi ukipata ajali ya aina yoyote na jino lako au meno yako ya mbele yakatoka?
Au inaweza isiwe ajali ila tu jino lako la mbele likaoza sana na likang’olewa kama sehemu ya matibabu?

Na hapo Labda wewe ni Mwalimu, Mwanasiasa, Mwandishi wa habari Jino la mbele limetoka au kung’olewa!? Na papo hapo Unasubiriwa katika semina au una kikao kazini,rafiki zako wanakuja kukusalimu au unatakiwa uende nje ya mkoa au nchi kwa haraka na meno/jino lako la mbele linalokupa muonekano limetoka!.

Je inawezekana kupata meno/ jino bandia kwa haraka? Jibu ni ndiyo inawezekana.

Matibabu haya yanaitwa kitaalamu IMMEDIATE DENTURE. Maana yake ni jino au meno bandia yanayo tengenezwa (fabricated) na kuwekwa kwa mgonjwa baada tu ya kung’olewa kwa meno asili.
Matibabu haya hutolewa siku hiyohiyo na daktari wa kinywa na meno baada ya kutolewa kwa jino/meno asili.

FAIDA ZA MATIBABU HAYA YA IMMEDIATE DENTURE.
1.Hurudisha muonekano mzuri wa mgonjwa.
2.Hurudisha uwezo wa kutamka vizuri maneno.
3.Ni rahisi jino hilo kutengenezwa kwa mfanano sawa na meno halisi yaliyopo kinywani.
4.Ni rahisi kwa mgonjwa kuyazoea meno/ jino bandia kwa haraka kama jino lake asili.
Jino bandia la haraka husaidia kulinda kidonda cha pengo kupona haraka.

HASARA ZA MENO BANDIA YA HARAKA.
1. Matibabu haya huchukua muda mrefu, hivyo mgonjwa husubiri sana hata saa moja na zaidi.
2. Mgonjwa atapata shida kidogo ya kutamka maneno kwa muda wa mwanzoni.

MAMBO YA KUZINGATIA BAADA YA KUPATA JINO/MENO BANDIA YA HARAKA.
1. Mgonjwa hatakiwi kuyatoa meno bandia kinywani kwa muda wa masaa 24.
2. Mgonjwa hatakiwi kutematema mate sana, hii inaweza kupelekea meno kupwaya.
3. Mgonjwa ale vyakula laini na si vigumu kwa kuanzia.
Baada ya masaa 24 mgonjwa anatakiwa kuyatoa meno bandia wakati wa usiku na kuyahifadhi katika maji masafi.

13 thoughts on “Jino langu limetoka, nitapata Jino bandia leo leo?

      1. Can I get more clarification plllz?? may b kma meno ya njano kma ya wachaga ambayo yameathirika na maji if am nat mistaken…yanaweza kua bleached?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show