Kwanini nimeze dawa za malaria wakati wa ujauzito?

Tafiti zinaonyesha kuwa Zaidi ya watoto laki mbili (200,000) hupoteza maisha kutokana na madhara ya malaria mara pindi wanapozaliwa. Mama mjamzito kutokana na kinga yake kuwa chini huwa kwenye hatari pia ya kupoteza Maisha kutokana na uginjwa huu hasa kwenye maeneo yenye maambukizi ya juu ya malaria kama India, Tanzania, Congo n.k

Dawa ya SP hutumika kama kinga kuzuia maambukizi ya malaria kwa mam wajawazito kwani inauwezo wa kukaa ndani ya mwili wa mam kwa wiki nne huku ikiendelea kumpatia kinga dhidi ya malaria yeye pamoja na mtoto aliyeko tumboni. Tafiti zimeonyesha kupungua kwa madhara na kuugua malaria tangu kuanza kutumika kwa dawa hii kwa wajawazito hivyo bado kuna umuhimu wa kuendelea kuitumia.
Licha ya kutumika kwa dawa hii bado kuna baadhi ya mama wajawazito hupata malaria ambapo dalili hizi zimetajwa kwenye kipengele cha chini;

DALILI ZA MALARIA KWA WAJAWAZITO
Dalili za ugonjwa huu kwa wajawazito na watu wengine huwa hazina tofauti yoyote isipokuwa zinaweza kuja kwa haraka Zaidi kwa wajawazito kutokana na kinga yao ya mwili kuwa chini na hivyo kuwa kali maradufu. Dalili hizo ni pamoja na; Homa, kichwa kuuma, mwili kuchoka , maumivu ya mwili wote, kutapika, kuharisha,kukosa hamu ya kula,kuongezeka ukubwa wa bandama pamoja.

MADHARA YA MALARIA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO

1 Upungufu wa damu Mimba kuharibika/kutoka
2 Kupungua kwa kiwango cha sukari kwenye damu Kuwahi kupata uchungu kabla ya muda
3 Manjano kwenye macho, Ngozi na kucha Mtoto kuzaliwa njiti
4 Figo kushindwa kufanya kazi Mtoto kufia tumboni mwa mama
5 Mapafu kujaa maji na kushindwa kupumua Mtoto kushindwa kukua tumboni
6 Degedege na kupoteza fahamu

MATIBABU YA MALARIA KWA WAJAWAZITO
Mara uonapo dalili tajwa hapo juu mama anashauriwa kuwahi mara moja hospitali kwanza apimwe ili kuthibitisha kama kweli ni malaria kwani kuna magonjwa mengine yenye dalili kama hizo.

Ikigundulika una tatizo hilo daktari atakupatia dawa kulingana na uzito wako huku akiangalia na umri wa ujauzito wako pamoja na hali yako ya ugonjwa.

Miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na Quinine kwa walio na umri wa mimba chini ya miezi mitatu, dawa mseto ya malaria (ALu) kwa walio na umri wa mimba zaidi ya miezi mitatu na nyingine kwa njia ya mshipa kama ni malaria kali.

ANGALIZO; mama mjamzito anapaswa kuzungumza na daktarin kabla ya kutumia dawa yoyote ili kupunguza madhara ya dawa kwake au kwa mtoto aliyetumboni yanayotokana na dawa hizo au muingiliano wa dawa hizo na nyinginezo anazotumia.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show