Jikinge na saratani

Mboga za majani kwa wingi katika chakula husaidia kujikinga na saratani. mboga hizo hufanya yafuatayo mwilini,

 • Zinalinda vina saba katika celi na kuzuia visiharibike
 • Hudhibiti chembe chembe ziletazo saratani zilizopo mwilini
 • Pia huzuia celi mwilini zisizaliane kwa wingi na kupelekea saratani
 • Huzuia uundwaji wa mishipa midogo midogo ya damu inayohitajika na celi za saratani
 • Pia huzuia kusambaa kwa saratani.

Mboga za majani hizo ni kama spinachi, brocoli na cabbage. Hivyo basi, hakikisha mlo wako unakuwa na walau kiasi kidogo cha mboga za majani ili kuepukana na janga hili. Saratani hasa ambazo zinaepukika kwa kula mboga za majani ni pamoja na,

 • Saratani ya tezi dume
 • Saratani ya utumbo wa chakula
 • Saratani ya matiti
 • Saratani ya mapafu

Pia utumiaji wa caroti, nyanya, biringanya na vitunguu katika mboga huzuia saratani

2 thoughts on “Jikinge na saratani

 1. Thank you for the article. How do u address the current situation in urban areas. Whereby urban small scale vegetable agriculture takes place. These vegetables are sometimes being watered (irrigated) with industrial waste water example from textile industries that contains harmful heavy materials which are said to be carcinogenic. These heavy metals bioaccumulate in the vegetables we eat everyday. Research has been conducted and it indicated presence of these carcinogenic heavy metals in vegetables. Different media had published. And its a challenge because some people are even resilient to eating vegetables. Unless they are sure where they are from.

  1. Ahsante sana kwa mchango wako ndugu Nuntwale. Ndio, Kuna Hilo jambo la watu kumwagilia mboga za majani na maji ambayo huwa ni majitaka kutoka kiwandani ambalo lipo hasa kwa sehemu za mijini. Ambalo kunakuwa na hatari ya binadamu kupata kemikali hizo pale atapotumia mboga hizo. Jambo ambalo kwa wale waishio mijini wanaweza kufanya ni pamoja na kupanda mboga mboga katika makopo na kuepukana na kumwagilia mboga hizo na maji taka kutoka kiwandani pamoja na kushinda kikwazo cha eneo kwa pamoja. Pia ni vyema ukawa na kitalu chako kidogo cha mboga mboga za majani mahala unapoishi, ili uwe na uhakika zaidi wa namna mboga zako zilivyomea. Kuliko kununua mboga za sokoni ambazo kwa kiasi kikubwa hutokana na maji hayo ya viwandani, hasa kwa wale waishio mijini. Kwani utumiaji wa mboga hizo badala ya kutoa saratani mwilini utakuwa umeileta mwilini kwako mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show