Nini nijue kuhusu saratani ya Mapafu

Saratani ya Mapafu ni aina ya saratani ambayo hushambulia mapafu na njia ya hewa  hivyo kuingilia mfumo wa kawaida wa upumuaji.Ni aina ya saratani ambayo imekuwa ikipelekea vifo vingi sana ambavyo kwa kiasi kikubwa vinaweza kuzuilika

Tabia hatarishi zinazopelekea kuongezeka kwa uwezekano wa kupata saratani hujumuisha zifuatazo

  • Uvutaji wa sigara. Moshi wa sigara una chembe chembe ndogo za nicotine ambazo hasa hupelekea kukua kwa saratani.
  • Kukaa karibu na mtu anayevuta sigara. Hii pia hupelekea kuvuta moshi anaoutoa mvutaji wa sigara. Na hivyo kupelekea na wewe kuongeza uwezekano wa kupata saratani
  • Kurithi. Hii pia ina nafasi kubwa sana ya kuongeza uwezekano wako wa kupata saratani. Kama ndani ya familia, Kuna ndugu wa karibu nae ameshaumwa saratani ya Mapafu, jua Kuna uwezekano na wewe ukapata pia
  • Asbestos. Hii ni aina ya chemikali iliyoko hasa kwenye vifaa vya kujengea. Hii pia imeonekana kupelekea kukua kwa saratani hasa kwa watu ambao wamekuwa wakitumia vifaa hivi kwa mda mrefu
  • Pia unavyokuwa na saratani sehemu nyingine ya mwili. Mfano, saratani ya shingo ya kizazi, au saratani ya ini. Kuna uwezekano mkubwa wa saratani hiyo kusambaa na kwenda kwenye Mapafu, hasa pale inapochelewa kutibiwa.
  • Kwa ujumla sababu moja pekee ina uwezekano mdogo wa kupelekea saratani, Bali zinapokuwa nyingi Kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata saratani.
MATUMIZI YA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show