Tatizo la fangasi ukeni limekua ni la kudumu kwangu

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, nimekua nikisumbuliwa na tatizo la fangasi ukeni kwa zaidi ya miaka 9 sasa. Sijui nifanye nini maana nimeshakata tamaa.

Kwa kawaida eneo la uke huwa na kiasi kikubwa cha bakteria (Lactobacillus) ukilinganisha na kiasi cha fangasi. Bakteria hawa wapo kwa ajili ya kudhibiti ukuaji wa fangasi na inapotokea mabadiliko kama matumizi ya antibayotiki kwa kipindi kirefu, kiasi kikubwa cha homoni wakati wa balehe na ujauzito au kushuka kwa kinga ya mwili sababu ya magonjwa kama kisukari au UKIMWI ndipo fangasi hawa hushamiri.

Fangasi aina ya “Candida albicans” ndiyo anayehusishwa zaidi na tatizo hili na huwakumba zaidi wanawake kati ya umri wa miaka 20-40.

Dalili ni zipi!?

  • Kuwashwa kunakoambatana na maumivu ukeni
  • Maumivu kama unaungua na moto wakati wa kukojoa au kufanya mapenzi
  • Kutokwa na uchafu mweupe, mzito, uliogandiana, usio na harufu na unaofanana na jibini (cheese).

“Ni muhimu kumuona daktari uonapo dalili hizi au zaidi kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi.”

Njia za kujiepusha

  1. Weka uke wako katika hali ya usafi; tumia sabuni isiyo na madawa makali kujisafisha kwa nje tu na jisuuze kwa maji ya kutosha.
  2. Baada ya kujisaidia jisafishe kutoka mbele kwenda nyuma kuzuia kusambaza vijidududu kutoka njia ya haja kubwa.
  3. Vaa nguo za ndani zenye uwezo wa kufyonza unyevu hasa zilizotengenezwa na pamba.
  4. Badilisha nguo zako mara tu unapomaliza kuogelea kuepusha unyevu.
  5. Zingatia ngono salama kwa kutumia kinga (kondumu).
  6. Badili pedi yako mara kwa mara unapokua kwenye hedhi.

“Tatizo la fangasi huwakumba watu wengi na huwa ni kero japokuwa habari njema ni kwamba linatibika na kuepukika”

9 thoughts on “Tatizo la fangasi ukeni limekua ni la kudumu kwangu

  1. Hongereni kwa kuamua kuelimisha jamii kwa njia hii.Naamini mtakuwa msaada kwa wanawake walio wengi.Kikubwa inabidi kuitangaza site hii ili wengi waweze kuifahamu na hivyo kunufaika nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show