Uhusiano kati ya utunzaji wa nafaka na saratani ya figo.

Mazao mbali mbali hasa ya chakula hupatikana kwa wingi wakati wa mavuno. Kutokana na upatikanaji huu wakulima wengi hukausha na kutunza mazao haya kwa njia mbali mbali ili yaweze kukidhi mahitaji ya chakula ya miezi ijayo. Pamoja na hayo watu wengi majumbani hununua nafaka kwa wingi wakati wa msimu ambapo bei ni nafuu na huyatunza majumbani kwao. Katika utunzaji huu ni muhimu kufahamu kuna aina ya fangasi aina ya Aspergillus ambae hushambulia mazao kama vile mahindi, maharagwe, karanga, mchele, ngano, mbegu za mafuta na viungo. Fangasi huyu huzalisha kemikali familia ya aflatoxin. Kemikali hizi huingiliana na mfumo wa protini na DNA mwilini na huweza kusababisha saratani ya figo kulingana na kiasi ambacho mtu amekula na muda ambao amekuwa akila nafaka zilizo shambuliwa na hawa fangasi.

Kuepukana na hili inashauriwa kufanya yafuatayo:
1. Chambua na kuondoa mazao yaliyoliwa na wadudu kwani mazao hayo yanauwezokano mkubwa zaidi wa kushambuliwa.
2. Kausha mazao vizuri kabla ya kuyatunza
3. Epuka kutunza mazao katika sehemu yenye unyevu na joto. Badala yake tafuta sehemu kavu yenye kuruhusu upepo kupita kwa ajili ya kutunza mazao
4. Iwapo kuna mazao ya kutunza muda mrefu ni muhimu kukagua mazao hayo mara kwa mara na kurudia zoezi la kuyaanika ama kukausha ili kuondoa unyevu wowote ambao unaweza kuwa umejitokeza.
5. Kila unapotumia mazao hakikisha unachambua vizuri na kutupa mazao ambayo yamebadilika rangi, yanautandu ama harufu inayoashiria mashambulizi.
Ni muhimu sana kuzingatia haya ilikujilinda dhidi ya saratani ya figo kutokana na kemikali hizi, kwani kemikali hizi zikishatengenezwa haziharibiwi na moto wala kuanikwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show