Zijue dalili za saratani ya mapafu

Saratani ya mapafu kwa watu wengi hukua bila kuonyesha dalili za awali na mgonjwa kupata dalili za saratani ikiwa imesambaa sehemu nyingine ya mwili.Endapo ukiona dalili na kumuona daktari mapema hupata matibabu na kuokoa maisha.

Dalili kwa mgonjwa wa saratani ya mapafu

 • Kukohoa mara kwa mara bila kupona au kupungua
 • Kukohoa damu au kohozi lililoambatana na michilizi ya damu
 • Maumivu ya kifua yanayoongezeka wakati wa kupumua au kukohoa
 • Sauti kuwa nzito ie kama kukoroma
 • Kupungua uzito na kukosa hamu ya kula
 • Kupumua kwa shida
 • Kuchoka na kuwa mdhaifu
 • Maradhi yanayojirudia katika njia ya hewa

Kama saratani ya mapafu itasambaa sehemu nyingine ya mwili hupata dalili zifuatazo;

 • Maumivu ya mifupa kama maumivu ya mgongo na nyonga ie.saratani kusambaa katika mifupa
 • Mabadiliko katika mfumo wa fahamu kama maumivu ya kichwa,kizunguzungu,kupoteza fahamu na ganzi katika mikono na miguu ie.saratani kusambaa katika ubongo au uti wa mgongo.
 • Manjano katika macho na ngozi ie.saratani kusambaa katika ini

Dalili hizi zinaweza kusababishwa na ugonjwa mwingine zaidi ya saratani ya mapafu nenda hospitali kuweza kujua sababu ya dalili na kupata matibabu.

MOSHI WA SIGARA UNA KEMIKALI ZAIDI YA 4000 NA KEMIKALI 43 ZINATAMBULIKA KUSABABISHA SARATANI

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show