Je, ni sawa kama mpenzi wangu hataki tutumie Kondomu?

Tuanzie na kuelimishana kondomu ni nini hasa? Kondomu ni nyenzo inayotumika katika kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa. Kuna kondomu za kiume na kondomu za kike: kondomu ya kiume ni nyembamba (kawaida hutengenezwa na mpira wa latex). Kondomu ya kike hutengenezwa kwa polyurethane na huwa na pete ili kuwa rahisi wakati inapokaa katika nafasi.

Unapofanya ngono, kutumia kondomu ni njia salama kabisa ya kujilinda pamoja na mpenzi wako dhidi ya magonjwa ya zinaa na mimba zisizo na mpango.

“Sijahitaji kondomu – nina afya salama?”
Huwezi kujua kama mtu ana maambukizi kwa kumwangalia – watu wengi wenye magonjwa ya ngono hawana dalili zinazoonekana kwa macho. Kama huwezi kuona vidonda vilivyo wazi, au uchafu na harufu mbaya haimaanishi kuwa mtu hana magonjwa ya zinaa.

“Sipendi kutumia kondom – huwezi kula pipi na ganda lake”
Ukiwa umevaa kondomu wakati wa tendo la ndoa huweza kukufanya usikie kawaida kama vile hujaivaa – jaribu kondomu nyembamba zaidi.
Kondomu pia huongeza hisia mpya kwa ngono. Kuna kondomu zinazokufanya wewe na mpenzi wako kuhisi hali ya joto katika tendo, pia zipo ambazo hufanya sehemu za siri kuonekana kubwa zaidi au kukusaidia kukaa kwa muda mrefu bila ya kufika kileleni. Kuna kondomu pia zenye vipele vipele vinavyosaidia kumpa mwanamke msisimko zaidi, na kondomu zenye rangi tofauti.
Kufanya ngono bila kondomu huweza kuonekana kuwa hali ya kawaida, lakini hukuweka wewe na mpenzi wako katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.

“Sitaki kuvaa kondomu – mimi hupoteza unyeti”
Ikiwa kondomu zimekufanya wewe au mpenzi wako kupoteza raha katika tendo katika siku za nyuma, angalia kondomu za aina nyingine zilizo nyembamba zaidi. Baadhi ni nyembamba sana na unaweza kujisikia kama hujavaa kabisa.
Vinginevyo, unaweza kutumia kondomu yenye vipelevipele ili kukuza msisimko kwako na kwa mpenzi wako. Watu wengine hupendelea kondomu zinazopunguza msisimko, ambazo zinaweza kuwa nzuri ikiwa una wasiwasi wa kufika kileleni mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show