Mambo 10 pengine ulikua huyafahamu kuhusu kisukari

Kisukari ni ugonjwa unaokuja kwa kasi katika jamii zetu kutokana na aina ya maisha tunayoishi katika nyakati za sasa. Mambo machache ningependa kukufahamisha au kukukumbusha kuhusiana na kisukari;

 1. Karibia theluthi moja ya watu wote wenye kisukari hawaja jijua kwamba wana tatizo hilo.
 2. Mara nyingi kisukari aina ya pili huwa hakioneshi dalili yeyote mpaka kufikia hatua za mbali.
 3. Asilimia 95 ya watu wote wenye kisukari wana kisukari aina ya pili.
 4. Endapo upo hatarini kupata kisukari kutokana na historia ya kisukari katika familia hasa aina ya pili, unaweza kukiepuka kwa kupunguza uzito na kuhakikisha unafanya mazoezi kila siku kwa muda usiopungua dakika 30.
 5. Mpango wa mlo kwa mtu mwenye kisukari hautofautiani sana na chakula kinachoshauriwa kuliwa na watu wasio na kisukari.
 6. Kisukari kinaongoza kwa kusababisha upofu baina ya watu wazima walio bado kwenye umri wa kufanya kazi.
 7. Watu wenye kisukari wana hatari mara mbili zaidi ya watu wasio na kisukari kupata magonjwa ya moyo.
 8. Udhibiti mzuri wa kiwango cha sukari katika damu unasaidia kujiepusha na madhara yatokanayo na kisukari na kuzuia madhara yaliyokuwepo kutozidi ongezeka.
 9. Watu wenye uzito mkubwa sana (obese) wakifanyiwa upasuaji wa tumbo unaoitwa “Bariatric surgery” husaidia kupunguza dalili za kisukari.
 10. Kisukari husababisha watu kutumia pesa nyingi sana kwa ajili ya matibabu kila mwaka.

2 thoughts on “Mambo 10 pengine ulikua huyafahamu kuhusu kisukari

 1. Asante kwa kutufunza;

  1. Vipi mwenye kisukari namba 2 je anaweza kujua kama anao ugonjwa huo ukiwa ktk hatua ya awali kwa vipimo hospitalini?

  2. Umeshauri mazoezi angalau dk 30 kwa siku, je ni lazima mazoezi hayo yafanyike kwa wakati mmoja kwa huo muda au unaweza kuyafanya hata kwa dk 15 asubuhi na dk 15 jioni?

  1. Asante kwa maswali Kaka Charles na ningependa kuyajibu kama ifuatavyo;
   1. Mtu mwenye kisukari aina ya pili hasa wale wenye uzito mkubwa mara nyingi huanza kuwa kwenye hatua inayoitwa “metabolic syndrome” ambapo mtu huwa na kiasi kikubwa cha mafuta na sukari kwenye damu. Kwa kufanyiwa vipimo ni njia rahisi kabisa ya kubaini endapo mtu ana tatizo hilo na hatua zikachukuliwa mapema.

   2. Siyo lazima ufanye mazoezi kwa mkupuo hizo dk 30 unaweza kufanya kidogo kidogo ingawa inapendekezwa ukianza hakikisha umetimiza walau dk 10, ukija badae unaongeza dk 10 nyingine mpaka unahakikisha ndani ya masaa 24 umetimiza zile dk 30 au zaidi.
   Endelea kufaidika na Daktari Mkononi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show