Tatizo la kusaga meno(Bruxism)

Baadhi ya watu wana  tabia ya kutafuna na kusaga meno yao bila wao kujua hasa wanapokuwa na hasira,msongo wa mawazo au wakiwa wamelala.Hali hii kitaalamu inajulikana kama bruxism. Mara nyingi  hali hii hutokea wakati wa usiku  (nocturnal bruxism) au hata wakati wa mchana.Tatizo hili  linahusianishwa na baadhi ya matatizo ya kisaikolojia na aina fulani za makundi ya tabia za watu,pia linaweza kuwa ni madhara ya pembeni(side effects) ya  baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili mfano antidepressants.

Zifuatazo ni dalili au namna ambavyo mtu anaweza kugundua kuwa ana tatizo la kutafuna au kusaga meno.

 • Kutoa sauti ya kusaga meno akiwa amelala,hii inaweza hata kumuasha mtu aliyelala na muhusika.
 • Meno kuonekana yamesagika,kulika au hata kulegea.
meno kuonekana yamesagika au kulika.

Mtu anaposaga au kutafuna meno wakati ambao hatafuni chakula au kitu chochote madhara kadhaa  yanaweza kutokea kama:

 • Kusagika kwa meno (attrition):  hii ni  kulika kwa meno kwenye sehemu ambapo meno ya juu na chini yanakutana (occlusal surface).
 • Ganzi au maumivu ya meno (sensitivity) wakati wa kunywa vitu vya baridi,kulingana na kiwango cha uharibifu wa meno yaani kusagika na kuisha kwa sehemu yote ya nje ya meno (enamel) na kufanya sehemu za ndani zinazofuatia kuguswa (dentine) au mzizi wa jino (pulp exposure).
 • Kulika kwa sehemu za  juu za kutafunia kwenye magego na visaidizi vyake(molars and premolars) na sehemu za kukatia kwa meno ya mbele(canines and incisors).
 • Kuchoka kwa misuli wakati wa kutafuna na wakati mwingine misuli hii hutanuka  na kunenepa kutokana na misuli hiyo kutumika zaidi(masseter muscle).
 • Maumivu kwenye  maungio ya  taya ya chini na fuvu (temporomandibular joint), kutoa sauti wakati wa kufugua na kufunga mdomo na wakati mwingine  kufyatuka kwa jointi hiyo (TMJ dislocation).

Matibabu ya tatizo hili yanatolewa na daktari wa kinywa na meno.

 • Kwa kwale ambao wana msongo wa mawazo wanashauriwa kupunguza mawazo,kupumzisha akili na kupatiwa ushauri na wataalamu wa saikolojia.
 • Mazoezi ya kulegeza taya(relaxation exercises)na kuachanisha meno kila mgonjwa anapohisi yanakutana yanaweza kusadia kupunguza tabia hii.
 • Kwa wale ambao ni vigumu kuacha tabia hii wanaweza kutengenezewa kifaa maalum cha kulinda meno wakati wa usiku(night guards),ambacho huvaliwa usiku wakati mgonjwa anapolala ilia kuzuia meno ya juu na ya chini kugusana.
kifaa maalumu anachopewa mgonjwa,kinavaliwa wakati wa kulala(night guard)
 • Mgonjwa akiacha tabia ya kusaga basi matibabu ya kurekebisha madhara yanaweza kufanyika kwa kuziba,kuua mzizi wa jino na kuvalisha meno kofia ngumu(hasa metal reinforced porcelain crown).
kuziba,kuvalisha kofia ngumu za metali kwenye meno.

Ni vizuri kumuuliza mwenzako kama amewahi kukusikia ukisaga meno usiku ili uweze kuchukua hatua za kuwaona wataalamu mapema.Kumbuka kujua tatizo mapema na kulitibu ni sehemu ya hatua ya kinga.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show