Unazijua njia 5 za kukuzuia kukoroma usingizini?

Kukoroma ni nini?

Kukoroma hutokea pale hewa inaposhindwa kupita kwa urahisi katika njia ya koo na pua ukiwa umelala

Je, ni njia zipi zinazoweza kunipunguzia hali hii?

1. Kuzingatia uzito na mlo bora. Kuwa na uzito mkubwa(unene) huweza kusababisha kukoroma. Mafuta yaliyozunguka shingo hupunguza njia ya hewa na kuzuia hewa kupita kiurahisi kutoka nje au kuingia ndani.

2. Jaribu kulala kwa ubavu badala ya kulala kwa mgongo. Wakati wa kulala kwa mgongo, ulimi wako au tishu yoyote ya mafuta huweza kulalia ama kukandamiza na kuziba njia ya hewa. Kulala kwa ubavu huzuia hii.

3. Usinywe pombe kabla ya kwenda kulala. Pombe hufanya misuli yako kupumzika zaidi kuliko kawaida wakati wa usingizi.

4. Acha kuvuta au punguza uvutaji wa sigara. Moshi wa sigara huathiri njia ya hewa katika pua na koo, na husababisha uvimbe. Hii husababisha kupungua kwa njia ya hewa na kusababisha kukoroma.

5. Hakikisha pua zako zipo wazi. Ni vizuri upumulie pua yako badala ya mdomo wako. Ikiwa kuna vikwazo vinazuia pua yako ni vizuri kumuona daktari wako, huweza ukawa na allergy au matatizo mengine yanayo jirudia mara kwa mara kama mafua vinjama vya puani(nasal polyps).

2 thoughts on “Unazijua njia 5 za kukuzuia kukoroma usingizini?

  1. Ni Kweli kabisa tatizo hili linahusiana kwani kuacha mdomo wazi hiweza kusababisha ulimi kurudi nyuma na kuziba njia ya hewa. Pia kupumulia mdomo hummpa mtu oxygen kidogo ukilinganisha na kupumulia pua. Hii pia inauhusiano na kukoroma.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show