Fahamu kuhusu leukokoria (Macho ya paka)

Hii Ni ishara ya kitabibu ambayo huonekana baada ya mwanga kumulikwa mbele ya macho kwa kifaa maalumu (Pen torch) na daktari.

Inaweza pia kugundulika wakati wa kupiga picha kwa bahati tuu

Macho ya kawaida hutoa rangi nyekundu/machungwa baada ya kumulikwa na kuashiria macho yako vizuri (Red reflex test)

Kama macho yatatoa mwanga mweupe (white pupillary reflex) baada ya kumulikwa huashiria Kuna tatizo la leukokoria ambayo Kama haitatibiwa mapema huweza kuleta matatizo ya kuona baadae katika maisha ya mtoto

Kuna magonjwa zaidi ya 10 yanayoweza kuleta ishara ya leukokoria kwa watoto lakini magonjwa mawili makubwa yanayotokea kwa Sana hasa katika jamii yetu Ni saratani iitwayo Retinoblastoma na Mtoto wa jicho (Cataract)

Retinoblastoma husababisha uvimbe ndani ya macho na Kama hautapatiwa matibabu mapema huweza kuleta upofu au hata kusambaa nje ya macho

Kwa nchi zilizoendelea wauguzi hufanya kipimo hiki Cha macho mapema kujua matatizo ya kuzaliwa yanayohusu macho na kuambatana na leukokoria

Kwa hapa nchini bado uelewa sio wa Hali ya juu lakini jitihada zinafanyika kuelimisha wauguzi wafanye kipimo Cha macho ili kuokoa macho ya mtoto na maisha kwa ujumla

Kwa wazazi na walezi uonapo ishara ya leukokoria yaani macho kuwaka kama ya paka hasa wakati wa usiku kwenye macho ya mtoto fika kituo Cha afya haraka iwezekanavyo

 

1 thought on “Fahamu kuhusu leukokoria (Macho ya paka)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show