safisha ulimi wako epuka harufu mbaya ya kinywa.

 

Machapisho mbalimbali yanaonesha kuwa karibia asilimia 90 ya watu wenye tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni(halitosis) huwa ni kutoka kwenye kinywa na meno,na kati ya hao asilimia 50 huwa ni kwa sababu hawasafishi ulimi vizuri.

Ulimi unaweza kutunza mamilioni ya bakteria kwa upande wake wa juu hii ni kutokana na mabaki ya chakula tunachokula na bakteria kuozesha mabaki hayo kutengeneza kemikali mbalimbali ikiwemo zenye mchanganyiko wa sulphur,hizi hutoa harufu mbaya na wakati mwingine huwa haivumiliki.

Dalili za kuwa hausafishi ulimi wako vizuri

 • Ulimi wako kuwa na rangi nyeupe,maziwa,njano au hata kijani kwenye eneo la juu(dorsum),unaweza kutumia kioo kuona mwenyewe.Kawaida ulimi unatakiwa kuwa na rangi ya pinki.
 • Kwa kutumia kijiko kwangua taratibu sehemu ya juu ya ulimi wako ukiona uchafu unabakia kwenye kijiko basi jua usafi wako ni hafifu na inawezekana kabisa kuna wakati fulani huwa unatoa harufu mbaya mdomoni.
ukikwangua na kupata uchafu wa hivi yawezekana una tatizo la harufu mbaya ya kinywa.
 • Kutokwa na harufu mbaya ndani ya dakika chache baada ya kupiga mswaki,inamaanisha umesafisha meno tu ukasahau ulimi.

Namna ya kusafisha ulimi vizuri.

Kwa kutumia mswaki wako au vifaa maalumu vya kusafishia ulimi(tongue scapers) safisha ulimi wako taratibu,unashauriwa kutumia dawa ya mswaki pia.

Inama mbele kidogo wakati wa kusafisha ulimi.
 • Unashauriwa kuinama kidogo kwenda mbele yaani kichwa kiwe mbele kuliko sehemu zingine za mwili na ingiza mswaki taratiibu mpaka eneo la ndani kabisa ambako mswaki hauendi ndani zaidi na safisha kuanzia hapo kuja nje,usitumie nguvu sana wala usijilazimishe kutapika.
mfano wa tongue scrapers kwa ajili ya kusafisha ulimi.

Inashauriwa kupiga mswaki vizuri angalau mara 2 kwa siku bila kusahau kusafisha ulimi,lakini kama una tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni na umejitahidi kusafisha ulimi wako vizuri na halijaisha usisite kumtembelea daktari wa meno kwa msaada wa kitaalamu inawezekana kukawa na sababu nyingine kama ilivyoelezwa kwenye makala yetu ya tatizo la kutokwa na harufu mbaya mdomoni.Jenga utaratibu wa kufanyiwa uchunguzi wa kinywa na meno angalau mara 2 kwa mwaka ili kupatiwa elimu na matibabu kila inapohitajika.

8 thoughts on “safisha ulimi wako epuka harufu mbaya ya kinywa.

  1. asante Happi kwa swali zuri,kuwa na geographical tongue peke yake siyo sababu ya kutokwa na harufu mbaya mdomoni,labda kama inatokea mtu ana geographical tongue na fissured tongue kwa pamoja ambayo hubakiza mabaki ya chakula kwenye vishimo au kukiwa na maambukizi na mtu kushindwa kusafisha ulimi vizuri kutokana na maumivu.karibu sana daktarimkononi.

  1. sijaelewa umemaanisha kutoka damu sehemu gani ya mdomo,ila kama ni kutokea kwenye fizi inawezekana kabisa kutokwa na harufu mbaya mdomoni kwani hizi ni hatua za mwanzo magonjwa ya fizi ambayo hasa husababishwa na usafi hafifu wa kinywa hivo wengi wao huwa pia wana tatizo la kutokwa na harufu mbaya,lakini kutokwa na damu mdomoni siyo dalili nzuri ni vizuri kutembelea kliniki ya meno iliyopo karibu na wewe ili kupatiwa msaada.Karibu tena daktarimkononi tukuelimishe.

 1. Shukrani kwa somo jipya Dr. maana wengi tumezoea kuelimishwa juu ya kusafisha meno elimu ambayo bado pia haijawafikia wengi juu ya usafishaji sahihi…

  Swali langu, je kutokusafisha ulimi kwa muda mrefu kuna madhara mengine zaidi ya harufu?

  1. asante kwa swali zuri Charles,hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kutokusafisha ulimi na magonjwa mengine ya kinywa,ingawa ulimi mchafu unaweza kuwa ni sehemu nzuri kwa vijidudu vya magonjwa kuweka makazi,hivo pamoja na kutokwa na harufu mbaya,unaweza hata kubadilisha ladha ya chakula pindi uchafu unapozidi,lakini ni rahisi kuambukiza maginjwa pale unapopata kidonda mdomoni au kwenye ulimi hivo kinaweza kuchelewa kupona.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show