Kwa nini watu wengi wenye kisukari wana shinikizo la damu pia? Na nini cha kufanya ili kuepuka hali hiyo?

Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya kisukari na shinikizo la damu, takribani asilimia 75 ya watu wenye kisukari hupata shinikizo la damu. Presha ya damu haitakiwi izidi 130/80 mmHg kwa wagonjwa wa kisukari.

Kwa namna gani kisukari kinapelekea shinikizo la damu?

-Kuamshwa kwa mhimili wa homoni zinazosimamia presha ya damu, mfumo huu kitaalamu unajulikana kama RAAS(Renin-Angiotensin-Aldosterone-System)

-Ongezeko la maji mwilini kwa sababu ya sukari kuwa nyingi

-Kupungua kwa ufanisi kazi wa sehemu maalum za mishipa ya damu kujua kama presha ya damu imepanda

-Mfumo wa fahamu unaohusika na shinikizo la damu kudhurika na kufanya presha ya damu isipungue wakati wa usiku

-Kisukari huathiri figo na presha ya damu kwenye figo, pia husababisha mishipa ya damu kuwa miembamba na kusababisha shinikizo la damu

Shinikizo la damu huleta madhara mengi sana kama vile kuathiri figo,ubongo,macho,moyo na kadhalika Pia huwa kuna changamoto zaidi katika kutibu shinikizo la damu kwa mtu mwenye kisukari ukilinganisha na asije na kisukari.

Hivyo basi ni vyema kuepukana na hili tatizo kwa njia zifuatazo

-Kuzingatia matibabu ya kisukari na kuonana na daktari mara kwa mara(Kliniki)

-Kula mlo unaoendana na kisukari

-Kuacha matumizi ya sigara

-Kufanya mazoezi

-Kuacha matumizi ya pombe

-Kuepuka matumizi ya chumvi kuzidi kiasi (sanasana chumvi mbichi)

Japo njia hizi zinasaidia kuepuka kisukari kupelekea shinikizo la damu lakini ni vyema kupunguza uwezekano wa kupata kisukari kwa kujiepusha na sababu hatarishi za kisukari kisicho cha kurithi(type 2 diabetes) kama vile kupunguza uzito, kula mlo bora na kuepuka matumizi ya pombe na sigara

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show