Ifahamu tiba aipatayo mtu alieng’atwa na mbwa

Majeraha yote yanayotokana na kung’atwa na wanyama yanapaswa kusafishwa vizuri kwa maji na sabuni.

Muathirika anapaswa apewe dawa ya antibayotiki kwa sababu majeraha hayo yana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi. Amoksilini yenye klavuliniki asidi inaweza ikawa moja wapo ya dawa hizo au pia klotrimozazo au metronidazo.

Kutibu majeraha yatokanayo na kung’atwa na mbwa;

  • Choma chanjo ya kichaa cha mbwa (rabies) na pia chanjo nyingine ya kusaidia kupambana na ugonjwa huo. Dawa hiyo huitwa dawa ya kichaa cha mbwa (antirabies/rabies immunoglobulin). Hii dawa ni salama zaidi ila pia ni ghali kuendana na mahali unapoishi.
  • Madhara ya pembeni ya hii dawa ni kama vile maumivu na sehemu sindano ilipochomwa kuvia na kuuma kwa ndani.
  • Sindano hiyo inabidi ichomwe eneo linalozunguka kidonda ambacho kimesafishwa. Pia inaweza ikachoma kwenye mkono wa juu kwnye misuli karibu na bega.
  • Kuna ukosefu wa dawa ya kutosha kwa ajili ya vidonda vyote? Unaweza kuongeza miyeyusho wa chumvi na maji (salini) kuzidisha kiasi kilichopo, angalau vidonda vyote vipate chanjo kiasi.
  • Sindano hizi huchomwa siku ya kujeruhiwa, baada ya siku tatu za kujeruhiwa, ikifwatiwa na: wiki ya kwanza, ya pili na ya nne baada ya siku ya kujeruhiwa.
  • Kama hukuwahi kuchoma sindano ya tetenasi au ulichomwa miaka mitano iliyopita, utahitaji kuchoma sindano hiyo ili kuongeza kinga ya mwili na vinyemelea hivyo.
  • Kama kidonda chako kitahitaji kushonwa, inashauriwa kutokutumia antiseptiki au antibayotiki ya kupaka mpaka muuguzi atakapokifanyia uchunguzi kidonda hiko.

Dawa hii pia inawza ikapewa kukinga maambukizi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa endapo utakua unahudhuria eneo lenye mbwa.

Muhimu:

Sindano hii inaweza kusababisha mzio mkali kwa baadhi ya watu. Wakati wowote unashauriwa kua na epinefrini/adrenalini karibu iwapo mzio utatokea

1 thought on “Ifahamu tiba aipatayo mtu alieng’atwa na mbwa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show