Je, nifanye nini ili niweze kumsaidia aliyeng’atwa na mbwa?

Mbwa ni wanyama ambao watu wengi tuna wapenda, kwani huwa ni wachangamfu sana kwa kucheza nasi na hata kuaminika kiasi cha kutumika kama walinzi majumbani kwetu katika nyakati za usiku. Lakini wanyama hawa bado ni hatari kwani mara kwa mara huweza kung’ata watu hasa watoto.

Huduma ya kwanza kwa mwathirika huwa kama ifuatavyo:

 • Kwanza kabisa hakikisha kwamba mazingira ni salama kwako, chukua tahadhari kwani mbwa huyo kama bado yupo katika mazingira hayo anaweza kukudhuru pia na wewe.
 • Tumia kitambaa, nguo au taulo safi kukandamizia sehemu aliponga’atwa muathirika ili kuzuia damu kutoka.
 • Pafunike sehemu ya kidonda alipong’atwa muathirika kwa bandeji au nguo safi na kisha mwahishe katika kituo cha afya au hospitali iliyopo karibu kwa ajili ya matibabu zaidi kama kupatiwa dawa na hata kushonwa kama sehemu alipong’atwa muathirika ni pakubwa.

Mambo muhimu ya kujua kabla ya kufika hospitali ambayo huweza kumsaidia sana daktari katika matibabu ya muathirika ni pamoja na:

 • Mmiliki wa mbwa huyo ni nani, na pia kama mbwa huyo amepata chanjo zote bila kusahau chanjo ya kichaa cha mbwa.
 • Ni muhimu pia kujua kama mbwa alimg’ata mtu huyo baada ya kuchokozwa au bila hata ya kuchokozwa.

Lakini pia ni vyema mapema kujiepusha na mazingira ambayo yanaweza kupelekea matukio kama haya kwani athari zake huweza kuwa kubwa kiafya. Zifuatazo ni njia mbali mbali ambazo unaweza kuzitumia ili kujiepusha na tukio kama hili:

 • Kaa mbali kabisa na mbwa usiowajua.
 • Usimwache mtoto peke yake na mbwa.
 • Epuka kucheza na mbwa anayekula au anayenyonyesha watoto wake.
 • Kama mbwa akiwa mkali au mwenye fujo, usikimbie wala kupiga kelele bali uwe mtulivu na uondoke katika eneo hilo taratibu bila ya kumuangalia mbwa huyo machoni.

Tukifanya hivi basi wote kwa pamoja tutashirikiana katika kutokomeza kabisa matukio haya katika jamii zetu.

4 thoughts on “Je, nifanye nini ili niweze kumsaidia aliyeng’atwa na mbwa?

  1. Asante kwa swali lako Chalo, kidonda pale ambapo atakapofika katika kituo cha afya au hospitali kabla ya kufungwa huwa pana safishwa na dawa na pia kabla ya kupafunga huwa panawekewa dawa kisha ndo panafungwa, hivyo husaidia katika kuzuia maambukizi ya bacteria kwa ujumla.

    1. Ndio Chalo ni vizuri kufunika kidonda kwa kutumia kitamba au nguo safi kabla ya kufika hospitali ili kusaidia kuzuia kidonda kisichafuke na kupata maambukizi. Karibu tena kwa swali lingine na endelea kufwatilia tovuti yetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show