Afya ya kinywa na meno kipindi cha ujauzito.

Kuna usemi miongoni mwa jamii yetu kuwa kila ujauzito huja na kung’oa/kuondoka kwa  jino. Dhana hii si ya kweli kwani yawezekana tatizo la jino lilikwepo hata kabla ya ujauzito.

Kipindi cha ujauzito ni kipindi cha muhimu sana kwa mama. Kipindi hiki huja na changamoto mbalimbali zikiwemo za kiafya. Matatizo na changamoto hizi hutokana na mabadiliko ya homoni mwilini. Mara nyingi matatizo ya afya ya kinywa na meno hayapewi kipaumbele kipindi cha ujauzito hivyo ni vyema mama anapoona dalili zozote za magonjwa hayo awasiliane na daktari kwa ajili ya ushauri na matibabu.

Je,matibabu ya kinywa na meno ni salama wakati wa ujauzito?

Ndio. Kwa wajawazito wengi matibabu haya ni salama. Ni vyema mama akamweleza daktari juu ya muda wa ujauzito wake, kama kuna  dawa zozote anazotumia,au kama ana matatizo yoyote katika ujauzito wake. Pia endapo kuna ushauri au tahadhari aliyopewa na daktari wake juu ya ujauzito huo.

Japokuwa wanawake wengi huweza kufikisha miezi tisa ya ujauzito bila kupata tatizo lolote la kinywa na meno ni vyema mama mjamzito amuone daktari wa meno pindi atakapogundua tatizo au mabadiliko yoyote kwenye kinywa chake, kwasababu mabadiliko ya homoni mwilini kipindi cha ujauzito huweza kupelekea mabadiliko katika kinywa.

Baadhi  ya mabadiliko  ya kinywa yanayoweza kutokea kipindi cha ujauzito  ni pamoja na;

  • Magonjwa ya fizi yatokanayo na ujauzito (pregnancy gingivitis). Ugonjwa huu hutokana na mabadiliko ya homoni mwilini na hauna uhusiano na ugonjwa wa fizi utokanao na uchafu wa kinywa (plaque). Fizi huvimba,huwa nyekundu na mara nyingne huwa na maumivu  na kutoa damu kidogo wakati wa kusafisha meno. Ni vyema mama akamuona daktari pindi apatapo tatizo hili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
  • Uvimbe utokanao na ujauzito (pregnancy tumour). Ugonjwa huu huwapata zaidi wamama katika miezi mitatu ya pili ya ujauzito (second trimester). Uvimbe huu hutoweka baada ya mama kujifungua lakini ni vyema mama akamuona daktari kwa uchunguzi na ushauri zaidi.

Ni vyema mama akazingatia ulaji wa vyakula vyenye virutubisho  kwani husaidia katika utengenezwaji wa meno ya mtoto. Vyakula vyenye vitamini A, C, na D, pamoja na vyakula vyenye protini na madini ya kalisi(calcium) na posferi (phosphorus) ni muhimu sana. Mama anashauriwa kujitahidi kupunguza kula vyakula vyenye sukari nyingi kwani huweza kusababisha kuoza kwa meno

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show