Matembele yanafaida gani katika mwili wangu?

Matembele ni mboga maarufu sana, pia ni mboga yenye virutubisho sana, mara nyingi watu hula mboga hii kwa msimu, kama inapotokea uchumi umeshuka nyumbani.. 😁😁 Lakini matembele yana faida nyingi katika miili yetu. 

1: Matembele yana madini ya chuma. Madini haya ndiyo muhimu katika utengenezaji wa damu, kwa hiyo mtu anapotumia matembele anakuwa anaongeza kiwango cha damu mwilini. Watu wenye upungufu wa damu na kina mama wajawazito wanashauriwa kula matembele kwa wingi.

2: Matembele yana vitamini A ambayo husaidia kuimarisha macho na hivyo kumsaidia mtu kuona vizuri hasa hasa nyakati za usiku.

3: Matembele yana vitamini C Ambayo humlinda mtu asipate kiseyenye (scurvy). Vitamini C huimarisha ngozi na fizi, unapotumia matembele fizi zako na ngozi huimarika na huzuia kuvuja damu kutoka kwenye fizi.

4: Matembele yana protini ambayo husaidia katika kuimarisha misuli na kusaidia katika ukuaji wa mwili.  Wape watoto matembele ili wakue vizuri.

Unajua jinsi ya kupika matembele kwa usahihi ili usiharibu virutubisho?  Fuatilia chapisho litakalo fuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show