Ntaipikaje mboga yangu ya majani ili nisipoteze virutubisho?

 1. Mboga za majani zina virutubisho vingi mno, Lakini jinsi ambavyo tunazipika tunaishia kupoteza virutubisho vyote. Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vya kuzingatia,
  1: Kabla hujaanza kuiandaa mboga, hakikisha hauiachi juani, iweke kivulini na uifunike vizuri. Kabla ya kuikata, toa uchafu kwa kuiosha na maji bila kuifikicha kwa nguvu.
  2:Katika uandaaji unapozikata mboga kumia kisu kikali, kwani unapotumia kisu butu baadhi ya madini hupotea wakati wa kukata.Pia maji ya kijani yanayotoka kwenye mboga hubeba madini, hivyo usiyamwage, pika pamoja na mboga yako.
  3: Pika mboga yako kwa dakika tano tu. Mara nyingi huwa tunapika mboga mpaka inabadilika rangi inakua ya kahawia. Upikaji huu sio mzuri kwa kuwa virutubisho vinapotea. Hivyo ni muhimu kuzingatia kupika kwa dakika zisizozidi tano.
  4: Funika mboga yako ilikuzuia virutubisho muhimu kupotea kwa njia ya mvuke.
  5: Unapomaliza kupika katika kula mboga za majani pamoja na mchuzi uliotoka kwenye mboga kwa sababu huo mchuzi unakua na madini mbalimbali.
  Ingawa madini yapo kwa wingi katika mboga za majani, pia mboga za majani husaidia kulainisha choo na hivyo kuepuka kupata choo kigumu.
  Kula mboga za majani.

2 thoughts on “Ntaipikaje mboga yangu ya majani ili nisipoteze virutubisho?

 1. Leo nimejifunza jambo muhimu sana,… Ili kujifunza zaidi naomba daktari unisaidie kunifafanulia yafuatayo;

  1. Kisu butu kinaondoa madini kwa namna gani hasa?

  2. Hayo maji ya kijani ni yale baada ya kuoshea mboga au? Na je haya uchafu na madhara?

  3. Je mboga itumie dk tano bila kujali aina na ukubwa wa moto?yaani moto wa kuni, mkaa, umeme au gesi?

  4. Na hizo dk 5 za mapishi ni pale pale tu ulipoweka chombo (sufuria) motoni au pale ulipotumbukiza mboga)? Na mboga iwekwe pindi unapoweka sufuria motoni au sufuria ikiishapata moto?

  5. Mwisho, je ni sahihi kupika mboga ya majani na viungo kama nyanya na vitunguu au bora zaidi upokee yenyewe? Pia ni vyema mkatuorodheshea na mboga majani bora zaidi kwa kufuata mtiririko wa ubora wake ili tujifunze mboga sahihi za kuzitumia

  1. 1: Kisu butu kina fanya mboga iwe ngumu kukatika na hivyo kujaribu kukata kata bila mafanikio kuna haribu mboga.
   2: Mboga yako ukishaiosha mara ya kwanza kabla ya kuikata ili kuondoa uchafu.
   Haya maji yakijani niliyoyaelezea ni ya kipindi cha kukata mboga.
   3: Moto wa wastani ndio unaohitajika kupikia mboga za majani, haijalishi unatumia chanzo kipi cha nishati.
   4: Dakika tano za kupika mboga ni kuanzia pale unatumbukiza mboga za majani zenyewe
   5: Ni sahihi maana vile ni viungo ambavyo vinaongeza ladha,muonekano wa mboga na hata hamu kwa mlaji. Ila kama unaweza kula bila viungo na yenyewe ni vizuri zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show