Ujumbe wa siku ya wanawake duniani 2018

Kuwa mwanamke ni tunu ya thamani na zawadi kubwa sana, sisi wanawake wa daktari mkononi tunajivunia hilo, na leo tunaungana na jamii na ulimwengu mzima kuwatakia heri ya siku ya wanawake duniani mwaka 2018.

Kwa namna ya pekee tunatamani jamii itambue ni kwa kiasi gani tunajiskia faraja kufika hapa tulipo leo. Wengi wetu wameanza kufikia ndoto zao wengine wamezikaribia na bila shaka kila mmoja wetu atafikia ndoto aliyoiota tangu akiwa mtoto. Tunatoa shukrani za dhati kwa wazazi, ndugu, jamaa, rafiki, walezi, walimu wetu na jamii nzima kwa kutuamini na kutupa nafasi ya kupata elimu na kujikomboa kifikra. Jamii inatuangalia kama madaktari, wafamasia na wataalamu wa afya, wazazi wetu na ndugu wanajivunia kuwa taifa linanufaika.

Leo kuna mtoto wa kike mahali ambapo ananyimwa nafasi ya kusoma na kufika hapa tulipo, wengine wananyanyasika na kuishia kupata mimba za utotoni na kushindwa kuendelea na masomo, wengine wanakatishwa tamaa kuwa hawawezi kusoma masomo ya sayansi, na vingine vingi lakini sisi tunasema kwa pamoja “Inawezekana kabisa kwa mtoto wa kike kulelewa vizuri, kupatiwa elimu na kuwa mwanamke bora hapo baadaye.” Ungana na sisi leo kuwa sehemu ya kuandaa kizazi cha wanawake wajao.

Tunaamini kuwa kila mmoja ana nafasi ya kushiriki katika kumwendeleza mwanamke na kumsaidia kufikia malengo yake.

  • Mwamini mwanamke,mpe nafasi
  • Mpende akiwa tangu mtoto lea ndoto zake
  • Mpatie elimu bora msaidie kufikia malengo
  • Shirikiana naye katika hatua zoteza ukuaji
  • Saidia biashara,kilimo na kazi zinazofanywa na wanawake
  • Tuwapende na kuwahishimu wanawake

Wanawake huleta chachu kwenye maendeleo ya jamii husika,mfano mzuri ni kama kina Dr.Avemaria Semakafu, mama Anna Makinda, Profesa Ndalichako, Ummy mwalimu na mama Samia Suluhu hawa ni wachache tu kwenye list ya wanawake wengi wa kitanzania walioweza kuwa na mchango mkubwa kwenye jamiii yetu.

Tunaungana na wanawake wengine dunia kwa kutoa elimu ya afya bure kabisa ili kuwasaidia ambao wanaikosa,lakini kuwapa hamasa wanafunzi wa kike na kuwaonesha kuwa hata wao wanaweza kufika wanapotazamia lakini tunapenda kuionesha jamii kuwa ukiwekeza kwa mwanamke umeliwekezea taifa zima.

#Press for progress kwenye nyanja zote za kiuchumi, siasa, elimu, utamaduni, ujasiriamali, urembo, ubunifu, familia na sehemu zingine zote tunazoweza kuzigusa. Happy women’s day.

4 thoughts on “Ujumbe wa siku ya wanawake duniani 2018

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show