Vijue vyakula vinavyosaidia katika tatizo la kukosa choo

Kukosa choo(constipation) ni moja  kati ya matatizo ya mfumo wa chakula yanayotokea mara kwa mara. Tatizo hili linawapata watu tofauti hasa watoto na wazee. Kukosa choo kunaweza kuwaa kuwa ni dalili ya tatizo kubwa zaidi kwenye  mfumo wa chakula.

Hali hii inasababishwa na vitu tofauti tofauti kama baadhi ya dawa, kutokula vyakula vya kutosha vyenye nyuzinyuzi,matatizo ya homoni, magonjwa mbalimbali katika mfumo wa chakula na hata mara nyingine  msongo wa mawazo.

Japokuwa ,kwa asilimia kubwa tatizo hili husababishwa na tabia za ulaji wa mtu kama kula vyakula vigumu na visivyo vya nyuzinyuzi hata kutokuwa na tabia ya kwenda chooni mara kwa mara(tabia ya kubana haja)

Mtu anayekosa choo mara nyingi huumwa tumbo,hupata choo kigumu na kidogo,huhisi tumbo kujaa na mara nyingine kuwa na tumbo kubwa.

Ufanye nini kujikinga na tatizo hili au kusaidia kulipunguza?..

-Kunywa maji ya kutosha haya husaidia katika mmng’enyo wa chakula . Maji yanatengeneza sehemu kubwa ya miili yetu na pia husaidia shughuli nyingi  mwilini.

-Kula matunda kama parachichi na mapapai kwa wingi.

-kula mboga za majani kwa wingi.

-Kunywa maziwa  mtindi hasa ule tunaotengeneza nyumbani na kama ni wa dukani basi iwe plain yoghurt hii husaidia kupata bakteria sahihi kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula.

Pamoja na vyakula, kufanya mazoezi ya kutembea na kuchuchumaahusaidia sana kwa kulainisha misuli na kuepusha michaniko na bawasiri(Kutokwa na kinyama kwenye njia ya haja kubwa)

Ikiwa umetumia vyakula hivyo bila kupata nafuu ,unaweza kwenda hospitali na kupewa dawa na kama bado dawa haitosaidia yaweza kupelekea upasuaji.

Tatizo hili likiachwa bila kutibiwa hupelekea kwa matatizo mengine mwilini ikiwemo kuoza kwa sehemu ya utumbo kwasababu ya mgandamizo wa mirija ya damu, kupata bawasiri na hata kupelekea maambukizi mwilini.

Kinga ni bora kuliko tiba,kula mlo kamili,mbogamboga za kutosha kunywa maji mengi,na nenda chooni kila unapohisi kubanwa na haja.

6 thoughts on “Vijue vyakula vinavyosaidia katika tatizo la kukosa choo

 1. Asante daktari, umeniongezea kitu maishani, ila naomba pia kuyafahamu yafuatayo;

  1. Je ni sawa zipi hasa kwa mifano ambazo huathiri choo?

  2. Pia umegusia homoni, je ni zipi na kwa namna gani zinahusika

  3. Mwisho umesemea magonjwa mbalimbali huweza kupelekea choo kukosekana, je ni magonjwa yapi hasa hayo?

  1. Habari kaka Charles,nafurahi sana pale unapojifunza na tunakushukuru kwa kutembelea tovuti yetu Mara kwa mara.
   1.sababu zinazoathiri choo mpaka kupelekea kukosa choo ni kama ulaji wa vyakula vigumu au visivyo vya nyuzinyuzi kama mbogamboga au kutokula matunda kwa wingi, utumiaji wa baadhi ya dawa kama morphine na Tramadol, minyoo,saratani ya utumbo mkubwa,matatizo ya kianatomia ya utumbo na pia kwa wagonjwa wanaokuwa wamelala kwa muda mrefu.
   2. Homoni nyingi huingiliana na mmeng’enyo wa chakula pale zinapokuwa nyingi au kidogo katika uzalishwaji mfano homoni ya thyroid hii ikiwa chini hupelekea upunguaji kazi za seli na hata kupunguza kazi ya utumbo mkubwa,pia homoni ya cortisol inapokuwa juu,homoni ya estrogen hasa kwa wajawazito na pale homoni ya insulini inapokuwa nyingi wakati wa kisukari inaweza pelekea kuharibu mishipa ya fahamu katika mfumo wa chakula na hivyo kuingilia utendaji kazi wa utumbo pia.
   3.Magonjwa kama kisukari,saratani ya utumbo mkubwa na magonjwa ya mishipa ya fahamu kama Parkinson
   Asante kaka,endelea kujifunza na kuwafahamisha wengine

  1. Habari Datuu shukrani sana kwa kutembelea tovuti yetu. Kwanza,wanawake wengi hupata hemorrhoid yaani bawasiri hasa katika kipindi cha miezi ya mwisho ya ujauzito hii ni kwa sababu ya kutanuka kwa mfuko wa kizazi na hali huzidishwa na uwepo wa kukosa choo pia.hivyo basi, hemorrhoid huwa na maumivu hata ikiwa mtu ameenda haja kubwa haya maumivu yanaweza kuwa makali zaidi wakati wa kujifungua na hivyo ni bora kujaribu njia za kupunguza kabla ya muda wa kujifungua.Njia hizi ni kama kujikanda na maji ya uvuguvugu au maji ya baridi na pia yaweza kuwa unaanza na maji ya uvuguvugu kujikanda halafu ya baridi.Njia nyingine ni kuhakikisha unajisafisha vizuri baada ya haja kuepuka maambukizi au kujiumiza zaidi.
   Asante sana ,endelea kujifunza.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show