“Daktari, Hizi ni Dalili za ujauzito?”

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25,siku 15 baada ya kupata hedhi yangu nilijamiana na mwenza wangu, sasa ni wiki ya 6 bado sijapata hedhi yangu na maziwa yangu yanauma sana, Je naweza kuwa mjamzito?

Wanawake wengi wamekuwa wanapata shida kujua dalili za mwanzo za ujauzito.

Kwa kawaida, msichana huweza kupata ujauzito pale anapojamiana siku za hatari katika mzunguko wake.

Dalili za ujauzito ni zipi?

Dalili za mwanzo za ujauzito ni :-

•Kutokupata hedhi zako zaidi ya mwezi mmoja.

•Maziwa kujaa na kuuma na pia eneo linalozunguka chuchu kuwa nyeusi zaidi.

•Kutokwa na ute mweupe mzito ukeni.

•Uchovu hasahasa kwenye wiki za kwanza.

•Homa ya asubuhi (Kusikia kichefuchefu na kutapika) hasa wiki ya 2 mpaka 8.

•Kuwa na hisia kali za harufu, baadhi ya harufu kukuletea kichefuchefu.

•Kupata haja ndogo mara kwa mara.

•Kuwa na hamu sana na baadhi ya vyakula na kuchukia vyakula vingine.

Dalili zilizochelewa za ujauzito ni:-

•Kuongezeka uzito.

•Kupata kiungulia.

•Kuvimba miguu.

•Kutokwa na haja ndogo ghafla baada ya kufanya vitu kama kupiga chafya, kucheka au kukohoa.

•Kukosa pumzi vizuri.

•Maumivu ya mgongo na kiuno.

Dalili za mwanzo za ujauzito zinafananiana na dalili hutokeazo siku chache kabla hujaanza siku zako za hedhi (Premenstrual syndrome), hivyo njia pekee ya kujua kwa hakika kama ni ujauzito au la, ni kujipima ujauzito uonapo dalili hizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show