KWANINI MWANANGU AMEFIA TUMBONI? (Sehemu B)

Moja Kati ya taarifa ngumu kupokea kwa mama mjamzito na familia kwa ujumla ni ile ya kifo cha mtoto akiwa tumboni. Ni wakati wa majonzi uliojaa maswali mengi ya nini kimetokea mwanangu akafa. Ziko sababu nyingi zinazoweza kupelekea mtoto kufia tumboni. Sababu hizi tunaweza kuzigawa katika makundi mbalimbali, katika toleo hili la pili tutaangalia namna ambavyo magonjwa ya mama mjamzito kama vile sukari na presha ya juu yanavyoweza kusababisha vifo vya watoto tumboni. 

•Mtoto hupata virutubisho muhimu kutoka kwa mama kupitia kondo la uzazi (placenta). Presha kubwa kwa mama mjamzito husababisha mishipa ya damu inayoenda katika mfuko wa uzazi kushindwa kupeleka virutubisho kwa mtoto na hii husababisha mtoto kushindwa kukua na huweza kuleta kifo kwa mtoto. Kifafa cha mimba pia huweza husababisha kifo kwa mtoto. ( Soma toleo kuhusu kifafa cha mimba hapa: http://daktarimkononi.com/2018/02/22/jekuna-tiba-ya-kifafa-cha-mimbanimechoka-kupoteza-watoto/

•Mama mjamzito kuwa na sukari ya juu katika damu (kisukari kisichodhibitika) pia ni moja ya sababu ambazo huweza kuhatarisha maisha ya mtoto tumboni. Sababu ya kisukari kuleta kifo kwa mtoto haijulikani ila tafiti huonyesha kuwa mama mjamzito mwenye sukari ya juu mwilini (kisukari kisichodhibitika) wana hatari kubwa ya watoto wao kufia tumboni.

•Magonjwa mbalimbali ya damu kama vile magonjwa ya kuvilia ( thrombophilia) yanaweza kupelekea kifo kwa mtoto akiwa tumboni hasa pale ambapo yanaposababisha damu kushindwa kumfikia mtoto kwa kutosha hivyo mtoto anakosa virutubisho muhimu na kupelekea kifo.

•Kuumia kwa mama mjamzito pia ni moja ya sababu zinazoweza kuleta kifo kwa mtoto akiwa tumboni. Ajali, kapigwa, kuanguka kunaweza husababisha hali hii. Sio Kila kuumia kwa mama mjamzito huleta kufa kwa mtoto tumboni lakini kuumia huongeza hatari ya mtoto kufa tumboni.

Ni habari mbaya kupokea kwamba mtoto amefariki tumboni. Ni wakati ambao mama anahitaji msaada kutoka kwa jamii inayomzunguka. Hii itamsaidia mama kurudi katika hali ya kawaida na kuepuka magonjwa mengine. Kama jamii ni jukumu letu kuhakikisha mama anakula chakula bora, anapata huduma stahili katika vituo vya afya. Ni vyema mama akapumzika kwa muda kabla hajapata mimba nyingine tena. Na anapokuwa mjamzito ni vyema kuhudhuria kliniki kwa wakati, kutibu magonjwa yoyote yanayomkabili mama, kujikinga na magonjwa wakati wa ujauzito, kufuata ushauri wa wataalamu wa afya hadi pale mtoto atakapozaliwa salama

 

Reviewed by Dr. Msiry

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show