Ujauzito: Kuna haja ya kula kwa wawili?

Watoto huzaliwa na magonjwa mbalimbali kwa sababu ya ulaji mbovu wa mama wakati wa ujauzito. Tabia ya “Kikija akilini, lazima kiingie tumboni” ina madhara makubwa sana kuliko tunavyodhani. Wanawake wengi hushauriwa kuwa wakati wa ujauzito, kila hitaji lake likidhiwe; akihitaji chakula chochote, hata kama kina madhara, apewe tu. Au huambiwa kula sana kupita kiasi, kwa kuwa analjilisha yeye mwenyewe pamoja na motto tumboni mwake. Huu si ushauri sahihi.

Ni kweli kuwa katika kipindi cha ujauzito, uhai wa viumbe viwili vipo mikononi mwa mama. Lakini, katika kipindi hiki, hasa kuliko kipindi kingine, hutakiwa kuwa mwangalifu sana kile anachokula, kisije kikahafifisha kwa njia yeyote ile nguvu za mwili na akili.
Ni utamaduni kutoa uhuru kwa mama mjamzito kula chochote na muda wowote kama anavyojisikia. Hii sio sahihi. Katika hali hii, hamu ya kula ya mwili hubadilika mara kwa mara na huweza kuwa ngumu kukidhi, hivyo mama hujikuta akijilisha mara kwa mara bila kujali kama kile anachokula kina manufaa mwilini au la.

Kama kuna kipindi kinachohitaji umakini katika ulaji ni kipindi cha ujauzito.

Si sahihi kutokuwa na tofauti ya mtindo wa maisha kati ya kabla na wakati wa ujauzito. Katika wakati huu, mabadiliko mengi makubwa yanaendelea katika mfumo wa mwili wa mama. Hii inahitaji damu nyingi zaidi hivyo mzunguko wa damu huhitaji kuongezeka. Hivyo huhitajika kuongezeka kwa chakula chenye afya ili kurutubisha damu. Bila lishe bora yenye kukidhi mahitaji ya mwili, mwili wa mama mjamzito hunyimwa ile asili ya uhai inayoipa nguvu mwili.

Nguo za mama mjamzito pia hutakiwa kuangaliwa kwa umakini. Mwili wake hupaswa kukingwa dhidi ya baridi, hasa sehemu za pembezoni za mwili kama mikono na miguu. Pia mama mjamzito hupaswa kupunguziwa kazi kwa kuwa kazi nyingi na kwa muda mrefu hulazimisha mwili kutumia virutubisho vingi kwa mama ili kuupa mwili wake nguvu, hivyo mtoto hunyimwa virutubisho hivyo.

Kama wewe ni mjamzito, hakikisha unajiwekea mpango mzuri wa kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya yako, pamoja na mtoto.
Punguza au epuka kutumia vyakula vyenye kusisimua, kwa sababu tu ina ladha nzuri. Lishe bora humaanisha kula vyakula vya aina mbalimbali ili kupata virutubisho tofautitofauti, na si mara zote humaanisha kuacha vyakula unavyopenda. Kula matunda na mbogamboga kwa wingi. Fanya mazoezi ya wastani mara kwa mara.

Linda afya yako kwa manufaa yako pamoja na ya mtoto!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show