Boresha afya ya uume wako kwa kuusafisha vyema

Uume ikiwa ni moja ya sehemu ambazo wanaume wanaithamini zaidi katika miili yao, ni muhimu basi kuiweka wakati wote katika hali ya usafi na yenye afya.

Jinsi ya kijisafisha uume

 • Osha uume wako taratibu kwa kutumia maji ya vuguvugu kila siku unapooga. Ikiwa una govi [foreskin] kwa kuwa hujatahiriwa, unatakiwa kuvuta ngozi ya govi nyuma taratibu na kusafisha chini yake vizuri kabisa.
 • Usipoosha chini ya govi husababisha uchafu kama jibini (cheese) kujikusanya na kuanza kutoa harufu mbaya, kufanya ngozi ya govi iwe ngumu kuirudisha nyuma na hata kusababisha bakteria kuzaliana. Hali ambayo inaweza kupelekea uvimbe kwenye kichwa cha uume na hii tunaita ‘Balanitis.’
 • Ikiwa ni mama anataka kumsafisha mtoto wake wa kiume anashauriwa asilazimishe kuirudisha nyuma ngozi ya govi kwa ajili ya kuisafisha kwa kuwa mtoto anapokua mdogo govi linaweza kuwa bado limejishikiza kwenye kichwa cha uume; hivyo kumuosha kwa nje tu inatosha.
 • Mara nyingi kuosha uume wako taratibu kwa kutumia maji ya vuguvugu  huwa inatosha kabisa. Ikiwa unapenda kutumia sabuni kwa ajili ya kujisafisha basi hakikisha haina madawa wala harufu kali ili kuepuka muwasho.
 • Mwisho kabisa usisahau kusafisha sehemu ya uume unapoanzia na korodani (testicles), ambapo jasho na nywele mahali hapo huweza kutengeneza harufu kali kama ya kikwapa kwa sababu huwa zinafunikwa na nguo ya ndani siku nzima.
 • Hakikisha eneo kati ya korodani na sehemu ya haja kubwa inasafishwa vizuri pia. Inapendeza ujisafishapo maeneo haya kujichunguza korodani zako kama kuna uvimbe hata mara moja kila mwezi.

20 thoughts on “Boresha afya ya uume wako kwa kuusafisha vyema

 1. Sio siri…navutiwa sana na mafunzo ya afya kutoka kwenu…much respect kwenu..Mola awabariki sana members wote mnaotoa elimu muhim kama hizi..

  1. Karibu tena Sarah
   Mwanaume anayetoa harufu huwezi kuhitimisha hapo hapo kwamba hajisafishi vizuri au la. Ikiwa Usafi wake wa uume ni duni bas inaweza kuwa ndiyo sababu lakini pia anaweza kuwa anasumbuliwa na magonjwa ya zinaa yakawa ndiyo yanamletea hiyo harufu mbaya. Kwahiyo ni vizuri aonapo kwamba kama shida yake ya harufu haisababishwi na Usafi basi atembelee kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
   Endelea kujumuika nasi katika tovuti yetu

 2. Asante Dr Beatha kwa elimu hii
  -Nakumbuka wakati nko o-level mwal wangu wa baiolojia alitwambia haifai kuosha testicles kwa maji ya moto, ila skuelewa kuna nini cha mno katika hili, maana watu wengu wakati wa baridi tunapenda kuoga maji ya moto.

  1. Asante sana ndugu kwa kuliibua hili maana umenikumbusha jambo muhimu nililotakiwa kulieleza.
   Kwanza kabisa inashauriwa unapoosha uume pamoja na korodani utumie maji ya vuguvugu kwani mbegu za kiume huweza kustahimili joto la mpaka nyuzi 35 na ndiyo maana korodani zimeshuka chini zaidi ya mwili ili kutengeneza mazingira mazuri ya mbegu kutengenezwa na kuhifadhiwa.
   Kujisafisha na maji ya moto kwa muda mrefu kunaweza kusababisha kuua mbegu na ndiyo maana tunashauri mtu atumie maji ya vuguvugu.
   Natumaini nitakua nimejibu swali lako; karibu sana

 3. Asante sana Dr.
  Na Je ? Kuna wadudu wanaopatikana kwa ukawaida wa kwenye uume. Kama tunavyosikiaga kuwa kuna wadudu wa kawaida wa Ukeni (nomoflora) kwa wanawake. Ningependa kujua kuhusu hili upande wetu sisi; wanaume.

  1. Asante Sure
   Kwa kawaida ngozi ya uume ni muendelezo wa ngozi ya mwili mzima hivyo basi normal flora wanaopatikana hapo huwa ni wale wale wa kwenye ngozi kama staphylococci, micrococci na diptheroids spp. Ingawa kwa wale wasiotahiriwa chini ya govi huwa na normal flora waitwao Mycobacterium smegmatis ambao huleta tatizo endapo utakua husafishi chini ya govi lako.
   Karibu tena Daktari Mkononi

  1. Shukrani Imma;
   Hakuna ulazima wa kusafisha uume tofauti na muda unapooga ila cha muhimu kuzingatia ni kuhakikisha unasafisha uume wako kila siku. Hata kama siku hiyo hujaoga ila kama ukumbukavyo kupiga mswaki kila siku basi kumbuka pia na kusafisha uume wako kila siku.
   Karibu kwa maswali zaidi

 4. Shukrani sana kwa funzo lako Dr. Beatha Mdendemi, maana limenisogeza hatua moja mbele ktk kuijali afya yangu. Nina maswali matatu kwako…

  1. Je vipi mtu anayeosha uume wake kwa maji ya baridi, kuna madhara? Na ni vyema basi tujue joto la maji lisipungue kiasi gani

  2. Huo ugonjwa wa “balanitis”je una madhara hasa zaidi kwa uume? Na je unatibika?

  3. Mwisho, je kuna madhara mengine yaani magonjwa mengine mtu anayoweza kuyapata kutokana na ukosefu wa usafi wa uume?

  ASANTE

  1. Asante Kaka Charles kwa maswali mazuri, majibu yake ningependa kuyatoa kama ifuatavyo:
   1. Umakini zaidi unaweka kwenye maji ya moto. Maji ya baridi kama hayakupi shida yeyote kuyatumia basi unaweza tu kuendelea nayo.
   2. Madhara yake usipotibiwa ni kufanya ngozi ya govi kugandia kwenye uume na hivo kuwa ngumu kuirudisha nyuma, mara chache mrija wa mkojo unaweza kuziba na kuleta shida kwenye Kukojoa. Tiba yake kwanza ni usafi wa uume, kuna dawa na pia kutahiriwa endapo mtu ana govi.
   3. Tatizo lingine analoweza kupata mtu akikosa usafi ni fangasi.
   Karibu tena

 5. Kuna madhara gani endapo mtu atatumia maji ya baridi kuosha uume wake?? (Chukua wakazi wa maeneo ya pwani kunakopatikana joto kubwa )

  1. Asante sana ndugu Bahati kwa swali zuri; maji yenye hatari ni yenye joto la juu linalozidi nyuzi joto 35, chini ya hapo hakuna madhara kabisa endapo ubaridi wa maji utamfanya mtumiaji awe comfortable.
   Karibu tena Daktari Mkononi na usikose kuwashirikisha wengine elimu hii. Siku njema

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show