Je wafahamu vichochezi vya saratani ya umio?

Kwa utangulizi,wagonjwa wengi wenye saratani ya umio huwa na upungufu wa lishe kwa sababu wanakuwa na ugumu kwenye kumeza(dysphagia)

VIFUATAVYO NI VICHOCHEZI VYA SARATANI HII:

 •  Umri kati ya miaka 45 mpaka 70.
 • Wanaume wanaadhiriwa mara 3 mpaka 4 zaidi ya wanawake.
 • Kuwa na tatizo la kucheua tindikali inayotoka tumboni (gastroesophagieal reflux disease) au tatizo la Barrett’s esophagus
 • Kuwa na uzito uliopitiliza na mafuta mengi mwilini.
 • Kupata tatizo la mishipa ya fahamu ya umio liitwalo achalasia
 • Maambukizi ya virusi aina ya human papilloma.
 • Uvutaji wa sigara wa muda mrefu
 • Utumiaji wa pombe kali kwa muda mrefu
 • Matumizi yasiyostahili ya asidi na tindikali (unywaji wa vitu kama maji ya betri)
 • Mionzi kwa ajili ya matibabu ya saratani nyingine vile vile huwa inachochea kutokea kwa saratani hii

  Ifahamike kuwa kuwa na sababu hizi haimaanishi moja kwa moja utapata saratani ya umio lakini hizi ni sababu tu ambazo zinaweza kupelekea kupata saratani hii,ni vyema kujiepusha na sababu hatarishi kama kuvuta sigara na unywaji wa pombe uliopitiliza .

 

 

1 thought on “Je wafahamu vichochezi vya saratani ya umio?

 1. Virusi aina ya Human papilloma virus (HPV) serotype 16 &18 pia vinahusishwa na saratani za koo..vinapatikana sana kwa kushiriki ngono kwa kutumia mdomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show