Najiandaaje kupokea majibu ya kipimo cha Saratani?

Wagonjwa 8 kati ya 10 wenye saratani barani Afrika hugundulika wakati ugonjwa huu umeshafika hatua za mwisho au umeshasambaa mwilini, mara nyingi kwa sababu ya uhaba wa vipimo au kutokuwa na tabia ya kupima mara kwa mara…

Mpaka kufikia maamuzi ya kwenda kwenye kituo cha afya kupima saratani ni hatua kubwa. Unastahili pongezi! Lakini baada ya vipimo, ufanye nini sasa?

Kuna njia mbalimbali za kujiandaa kupokea majibu ya vipimo vya saratani:
1. Baada ya vipimo kuchukuliwa, ulizia lini majibu yatakuwa tayari na jinsi utakavyoyapata.
Ukiona kimya kwa siku kadhaa baada ya siku uliyopewa, waweza kurudi hospitali kufuatilia majibu yako, kwa kuwa mara chache huweza kupotea.

2. Andika maswali yote ambayo ungependa kumuuliza daktari pindi yanapokuja tu akilini.
Mfano kama una saratani, ipo katika hatua gani, lini matibabu yanaanza, madhara na matokeo ya matibabu, pamoja na ushauri kwa ujumla. Ni rahisi sana kusahau ulichotaka kuuliza kwa sababu ya hali ya wasiwasi na mashaka wakati ukisubiri majibu.

3. Kuwa na mtu wa karibu atakayekusindikiza unapoenda kupokea majibu.
Huyu atakuwa msaada kwako kukushauri na kukutia moyo wakati upo katika hali ya woga, wasiwasi au mashaka.

4. Fahamu kuwa hakuna hisia sahihi ya kupokelea majibu.
Unaweza kuwa na mchangayiko wa hisia ikiwemo hofu, hasira, kujihisi upweke au hauwezi, kukataa majibu, msongo wa mawazo nk. Wengine huweza hata kuzimia. Cha muhimu ni kuweza kudhibiti hisia zako zisipitilize. Mtu wa karibu aliyekusindikiza anaweza kukusaidia pale unapolemewa na hisia.

5. Fuata maelekezo na ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Ushauri unaotolewa usipuuzwe, hata kama majibu yakiwa mazuri. Ukiweza, andika ili kuweka kumbukumbu ya kukusaidia kupitia baadaye wakati akili imetulia.

Anza kujenga tabia ya kupima afya yako mara kwa mara ili kama tatizo likiwepo, ligundulike mapema na kutatuliwa ipasavyo.

2 thoughts on “Najiandaaje kupokea majibu ya kipimo cha Saratani?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show