Ujue ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea), dalili zake na kinga.

Kisonono ni ugonjwa gani??

Kisonono ni moja ya ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria huyu hukua nakuzaliana kwa haraka kwenye maeneo yenye unyevu unyevu na joto mwilini kama sehemu ya ndani ya uke, kwenye shingo ya uzazi wa mwanamke (cervix), nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya kupitisha mayai (fallopian tube) mdomoni, kwenye puru (njia ya haja kubwa), pamoja na kwenye mirija ya kupitishia mkojo na shahawa (urethra).

Kisonono huambukizwaje?

Ugonjwa huu huambukizwa kwa kufanya ngono isiyo salama na mtu mwenye ugonjwa huu. Kisonono huweza kuambukizwa kwa kujamiiana kupitia njia ya kawaida (uke na uume), ngono ya mdomoni (oral sex), pamoja na ngono ya haja kubwa (anal sex).

Zipi ni dalili za kisonono?

Dalili za kosonono hutokea kati ya siku 2 mpaka 10 baada ya kujamiina na muathirika wa ugonjwa huu. Ila kuna wakati inaweza chukua mpaka siku 30 ndo dalili kuonekana, mara nyingi wanaume hua wanawahi kupata dalili hizi kuliko wanawake.

Dalili za kisonono kwa mwanaume:

 1. Kutokwa na majimaji meupe (usaha) au ya kijani kwenye njia ya mkojo (urethra discharge)
 2. Maumivu ya kuchoma choma na kuungua wakati wa kukojoa (burning sensation)
 3. Maumivu ya korodani na wakati mwingine kuvimba
 4. Kama maambukizi yapo kweye puru huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa ambapo mda mwingine damu inaweza onekana kwenye haja, pia muwasho wa njia hii.
 5. Maumivu ya kuchoma kooni (hii hutokana na maambukii kwa njia ya ngono ya mdomoni)
 6. Kuvimba kwa tezi za kooni (maambukizi kwa ngono ya mdomoni)

Dalili za kisonono kwa mwanamke:

 1. Kutokwa na majimaji ya njano au meupe ukeni (usaha)
 2. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
 3. Kutokwa na damu ukeni kabla ya siku za hedhi
 4. Kutokwa na damu baada ya kujamiiana
 5. Maumivu ya kuchoma kooni (hii hutokana na maambukii kwa njia ya ngono ya mdomoni)
 6. Kuvimba kwa tezi za kooni (maambukizi kwa ngono ya mdomoni)
 7. Kama maambukizi yapo kweye puru huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa ambapo mda mwingine damu inaweza onekana kwenye haja, pia muwasho wa njia hii.

Je tiba sahihi ya kisonono ni ipi??

Magonjwa mengi ya zinaa huwa na dalili za kufanana hivyo kwa tiba sahihi ya ugonjwa huu unashauriwa kwenda hospitali au kituo cha afya kwa ajili ya vipimo na dawa sahihi ya ugonjwa husika. Si vizuri kwenda kwenye maduka ya madawa moja kwa moja bila kwenda hospitali kwa sababu endapo utapewa dawa au dozi isiyo sahihi kuna hatari ya ugonjwa huu kua sugu.

Endapo sitatibiwa kisonono ni nini athari zake?

 1. Kisonono kisipotibiwa husababisha utasa kwa mwanamke na kwa mwanaume na kupotea uwezo wa kuzaa na kuzalisha.
 2. Huweza kuathiri valvu za moyo, ubongo na ngozi.
 3. Huweza kushambulia viungo vya mwili (inflammation of joints)
 4. Kwa wanawake wajawazito ugonjwa huu huongeza athari za kuzaa kabla ya muda (kabla ya miezi tisa), kupata mtoto njiti, pia wakati wa kujifungua mama mwenye ungonjwa huu anaweza muambukiza mtoto wake na hivyo mtoto anaweza kupata athari kama ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, upofu na homa ya mapafu.

Je nifanye nini ili nijikinge na ugonjwa wa kisonono?

 1. Kua na mpenzi mmoja na muwe waaminifu
 2. Tumia kondomu wakati wa kujamiiana.
 3. Nenda na mwenzi wako uliyejamiiana nae kutibiwa
 4. .Kwa wanawake wajawazito ni muhimu kuhudhuria kliniki kwa ajili ya vipimo na matibabu

Privacy Preference Center