Zifahamu dalili za awali za saratani

Saratani ni ugonjwa ambao huchukua mda mrefu hadi kugundulika. Na mara nyingi, mgonjwa akigundulika huwa katika hatua za mwisho za ugonjwa na hivyo kupelekea Hali ya ugumu katika matibabu yake.

Mbali Na hayo, Kuna dalili ambazo ukiziona zimedumu kwa mda mrefu ( takribani miezi mitatu au zaidi) zinaweza kuashiria hali ya hatari. Dalili hizo ni pamoja Na:

  • Kubadilika kwa hali ya upataji choo (kukaa mda mrefu sana Bila kupata choo au kuwa kama cha mbuzi)
  • Kuwa na kidonda mdomoni kwa mda mrefu sana ambacho hakiponi
  • Kutokwa na damu ukeni hasa baada ya tendo la ndoa kwa mwanamke ambaye ameshakoma hedhi (menopause)
  • Uvimbe usio na maumivu kwenye matiti
  • Kupata shida ya kumeza chakula hasa vyakula vigumu na baadae vyakula vilaini
  • Kubadilika kwa sauti na kuwa ya mkwaruzo kwa mda mrefu
  • Kikohozi cha mda mrefu kisichopona kwa dawa na pia kinaweza kuambatana na damu
  • Kupungua uzito bila kuwa na sababu maalumu

Ukiona dalili hizi haina maana kwamba utakuwa na saratani bali ina maana Kuna uwezekano wa wewe kuwa na saratani. Hivyo basi ni muhimu kwenda kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show