Fahamu nyoka 4 wenye sumu kali Africa

 

4. Gaboon Viper

Gaboon viper (Bitis gabonica) nyoka hawa huwa na meno marefu kuliko wengine yanayoweza kufika sentimita 5 kwa urefu. Tena ni nyoka mzito mno anayeweza kukua na kufika kilo 11.3 na urefu wa mita 1.5. hupatikana Afrika ya kati, mashariki na magharibi. Nyoka hawa huwinda usiku na hutoa sumu nyingi sana. Hata hivyo nyoka hawa hutembea polepole na hawang’ati kirahisi mpakawatakapochokozwa au kukanyagwa.

 

3. Boomslang (Dispholidus typus)

Nyoka hawa hupatikana kusini mwa jangwa la sahara. Sumu ya nyoka huyu huathiri mfumo wa kawaida wa mwili wa kuvia damu, hivyo mtu aliyeng’atwa hutoka damu bila kuzuilika. Dalili hizi huchukua muda kutokea na hivyo watu wengi hukosa huduma stahiki kwa wakati. Nyoka hawa hawaui watu wengi kwani wana tabia ya kukwepa binadamu na hukaa katika miti Nyoka hawa huweza kufika urefu wa mita 1.6

 

2. Puff Adder
(Bitis arietans) nyoka huyu husababisha vifo vingi zaidi, kwani hupatikana katika maeneo mengi na yenye watu wengi. Mbali na hapo, rangi zao huwafanya waendane na mazingira yao, hivyo watu wengi hung’atwa kwa kuwakanyaga bahati mbaya. Nyoka hawa husifika kuwa na sumu kali lakini vifo vingi zaidi ni hutokana na kukosa huduma sahihi. Urefu wao huweza kufika mita 1

  1. Ingawa black mamba sio nyoka mwenye sumu kuliko wote Afrika, bila shaka ni moja kati ya nyoka wanaoogopwa mno. Hii hutokana na tabia za nyoka huyu na ukubwa wake maana ni mkubwa kuliko wote barani Afrika,akiwa na urefu unaoweza kufika mita 2.5 na pia ni wenye mbio zaidi.
    Sifa yake pia ni uwezo wa kung’ata zaidi ya mara moja. Sumu yake huweza kumfanya mtu akapoteza fahamu ndani ya dakika 45 na bila matibabu kifo ni asilimia 100 ndani ya masaa 7 hadi 15. Sumu ya nyoka huyu hulenga mfumo wa fahamu na moyo.
    Nyoka hawa si weusi kama jina lao na hukaa katika ardhi na sio katika miti

Je unafahamu nini cha kufanya pale unapong’atwa na nyoka hawa? ingia katika link hii kujua huduma ya kwanza http://daktarimkononi.com/2018/02/14/huduma-ya-kwanza-kwa-mtu-aliyengatwa-na-nyoka/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show