Kwa nini siruhusiwi kula chochote kabla ya kufanyiwa upasuaji

Umewahi kujiuliza kwa nini Daktari hukwambia kutokula chochote walau masaa sita kabla ya kufanyiwa upasuaji? Inaweza ikawa wewe au ndugu yako unayemuuguza.

Sababu kubwa ni kuzuia chakula kurudi juu na kuingia katika mfumo wa hewa na kisha kuingia kwenye mapafu na kusababisha mapafu kuathirika na hivi kukupelekea shida kwenye kupumua pia inaweza kusababisha maambukizi kama pneumonia. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa.

Je, nini husababisha chakula kurudi juu na kuingia kwenye njia ya hewa?

Hii hutokana na dawa za usingizi (nusu kaputi) ambazo mgonjwa hupewa kabla ya upasuaji ili asisikie maumivu wakati wa upasuaji. Dawa hizi hulegeza misuli yote ya mwili ikiwemo ya tumbo, umio, koo na njia ya hewa na hivi misuli hiyo iliyolegea kushindwa kuzuia chakula kurudi kutoka mfuko wa chakula(tumbo) kupanda juu na kuingia njia ya hewa na hatimaye kwenye mapafu na kuleta athari izo.

Kwa nini kutokula masaa sita?

Hii huupa muda chakula kutoka katika mfuko wa chakula na kuingia katika utumbo mwembamba na kuelekea utumbo mkubwa na hivi hupunguza chakula kilicho katika mfumo wa chakula. Hii hupunguza na kuzuia kabisa nafasi ya uwepo wa chakula katika mfuko wa chakula ambacho kinaweza rudi katika mfumo wa hewa na kuingia kwenye mapafu pale mtu anapewa dawa ya usingizi.

Siruhusiwi kunywa hata maji?

Maji huruhusiwa mpaka masaa mawili kabla ya kufanyiwa upasuaji. Masaa sita ni kwa ajili ya vyakula.

Nifanye nini ikiwa nimekula?

Usione aibu kumwambia daktari wako kabla ya kufanyiwa upasuaji kama umekula ndani ya masaa hayo ambayo hukutakiwa kula ili kuepuka madhara hayo.

 

 

2 thoughts on “Kwa nini siruhusiwi kula chochote kabla ya kufanyiwa upasuaji

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show