Nini kifanyike ili kusafisha uke na kuuacha ukiwa wenye afya!?

Uke ulivyoumbwa ulitengenezwa kwa ajili ya kujisafisha wenyewe kwa msaada wa ute asilia unaotengenezwa kutoka kwenye kuta zake na shingo ya uzazi. Uke huanzia kwennye shingo ya kizazi mpaka kwenye uwazi unaonekana kwa nje.

Ukiachana na damu anayotoka mwanamke wakati wa mzunguko wake wa kawaida wa hedhi; si jambo la kushangaza kwa yeye kutokwa na ute mweupe au kama maji kutoka ukeni. Mabadiliko katika wingi wa ute huu huendana na mabadiliko ya homoni kwenye mwili wake wakati wa mzunguko wa hedhi, ujauzito au ukomo wa hedhi.

Wakati mwingine ute huu hubadilika na kuwa mzito na unaovutika na huu huwa ni wakati yai linatolewa kwenye ovary (ovulation). Wakati wote huo zingatia kwamba ute wa kawaida huwa hautoi harufu kali wala rangi tofauti na rangi tajwa hapo juu. Endapo utaona mabadiliko ya ute tofauti na ulivyozoea wewe hasa kwenye rangi, harufu au kuleta muwasho, tafadhali tembelea kituo cha afya.

Jinsi ya kujisafisha uke

 • Unachotakiwa kuosha wewe mwenyewe ni sehemu ya nje inayozunguka uke yaani mashavu [vulva] maana sehemu ya ndani inajisafisha yenyewe.
 • Muhimu ni kuhakikisha unajisafisha kila siku kwa kutumia sabuni isiyo na madawa au harufu kali kwani huweza kuua bakteria wanaolinda uke ambayo inaweza kupelekea kwa baadhi kupata muwasho au ukuaji wa fangasi, baada ya hapo jisuuze vizuri kwa maji ya kutosha kuondoa sabuni yote.
 • Ni muhimu pia kusafisha eneo lililopo kati ya uke na sehemu ya haja kubwa kila mara unapooga kuepuka kutunza uchafu.
 • Wakati wa hedhi inashauriwa kujisafisha zaidi ya mara moja.

6 thoughts on “Nini kifanyike ili kusafisha uke na kuuacha ukiwa wenye afya!?

  1. Asante sana Sarah; kama nilivoeleza kwamba uke huwa unajisafisha wenyewe na wewe jukumu lako ni kuusafisha tu kwa nje. Unapoingiza kidole kwa lengo la kusafisha kwanza unaweza kuwaondoa bakteria asilia wanaoishi kwenye uke ili kuulinda na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata mashambulizi ya wadudu wengine kama fangasi. Pili kidole chako kinaweza kisiwe kisafi kwa kiwango cha kutosha na hivyo kupelekea wewe mwenyewe kujiingizia vijidudu kwenye uke wako.
   Natumaini nimejibu swali lako; karibu tena Daktari Mkononi

 1. Dr. Mdendemi, ubarikiwe kwa elimu hii kwa dada zetu, japo mie sihusiki na hii mada ila nilipenda kuuliza kwa lengo la wanawake kujifunza

  1. Umesema eneo la ndani uke hujisafisha wenyewe, ni vyema pia wanawake wakajifunza na namna tendo hilo la kujisafisha lenyewe linavyofanyika

  2. Je hao bakteria wanaolinda uke, je hawana madhara yoyote au ya namna nyingine kwa mwanamke?

  3. Huo ulinzi wa bakteria hufanyika kwa namna gani na dhidi ya nini?

  4. Nini madhara ya kutokujisafisha uke, kutokusafisha kwa wakati na matumizi ya sabuni zisizo sahihi?

  5. Mwisho, je ni kiasi gani cha maji kinachofaa kutumika, idadi ya usafi wa uke kwa siku na pia aina ya maji aidha ya moto, baridi au vuguvugu yanayopaswa kutumika?

  1. Kwa maswali haya nitayajibu hivi;
   1. Uke hujisafisha wenyewe kwa kutumia ute unaotengenezwa kwenye shingo ya kizazi na kuta zake. Ute huo unavotoka ndipo hutoka na uchafu uliopo
   2. Hawana madhara yeyote kama watakua katika kiwango kinachostahili kwani hapo ndipo mahali pake pa kuishi na wapo hapo kwa lengo maalumu la kuzuia ukuaji wa vijidudu wengine.
   3. Uwepo wa hao bakteria kwenye eneo Hilo Ndiyo huwa ulinzi kwani huzuia nafasi ya vijidudu wengine kuwepo. Na mara nyingi ulinzi wao huwa ni dhidi ya fangasi.
   4. Kutojisafisha uke huleta harufu mbaya na kutengeneza mazingira kwa ajili ya vijidudu kukua. Kujisafisha kwa sabuni zisizostahili huleta muwasho kama irritation ambao siyo wote wanaweza kupata lakini maana kuna wanaotumia sabuni hizo na hawapati madhara.
   5. Maji yanayotakiwa ni kiasi cha kutosha kuhakikisha umeondoa sabuni yote. Inashauriwa ujisafishe kila unapooga na mara nyingi zaidi ikiwa ni kwenye siku zake. Maji yanayotumika kwa mwanamke ni ya joto lolote ataloona yeye linamfaa

 2. Je ni sabuni gani ambazo zinashauriwa kutumika kusafisha uke maana kuna baadhi ya madaktari wanapinga utumiaji wa sabuni kabisa.

  1. Sabuni zipo nyingi, cha muhimu kuzingatia ni kuhakikisha siyo medicated maana medicated soaps zipo kwa lengo la kuua vijidudu. Wengine hushauri watu wasitumie sabuni kwa sababu siyo rahisi kuhakikisha haujiingizii sabuni hata kidogo.
   Karibu tena Daktari Mkononi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show