Tatizo la kufika kileleni mapema kwa wanaume

Kufika kileleni mapema ni tatizo kubwa kwa wanaume. Wastani wa muda unaotumika kwa wanaume wengi wakati wa kujamiiana ni dakika tano na nusu hadi dakika kumi. Hata hivyo, ni juu ya wapenzi kuamua muda gani wanaridhika nao – hakuna ufafanuzi halisi wa muda gani ni sahihi na unatosha.

Matukio ya kufika kileleni mapema ni ya kawaida na haitakiwi kuleta wasiwasi. Lakini ikiwa karibu nusu ya tendo la ngono hutokea ukimwaga mapema, hili linaweza kuwa tatizo.

Sababu gani husababisha hali hii?

Sababu mbalimbali za kisaikolojia na za kimwili zinaweza kusababisha kufika kileleni mapema.

Sababu za kimwili ni kama:
* matatizo ya tezi dume
* matatizo ya tezirosi (thyroid)
* kutumia madawa ya kulevya

Sababu za kisaikolojia ni kama:
* sonona (depression)
* msongo wa mawazo (stress)
* matatizo ya uhusiano na mpenzi
* wasiwasi juu ya utendaji wa ngono (hasa katika mwanzo wa uhusiano mpya, au wakati mtu amekuwa na matatizo ya awali na utendaji wa ngono)
* Ulelewaji unaopinga kabisa maswala ya mapenzi na ngono

16 thoughts on “Tatizo la kufika kileleni mapema kwa wanaume

 1. Aisee hii kali kweli…Dr naomba kuuliza relationship kati ya masturbatin na kuchelewa kufika kileleni ni hasa sababu…na pia huoni kwamba hii inaweza kuwa ni moja ya sababu ya ku abuse masturbation?

  1. Tendo hilo la kujichua linapunguza hamu baada ya kukimaliza, ndio maana hutumika. Hapa tatizo kubwa zaidi ni kufika kileleni mapema na hivyo inabidi tuangalie tatizo kubwa zaidi lipo wapi!

 2. One Physical exercise training called kegel for PC- muscles has shown greater semi permanent improvement you should consider it.

 3. Is this true Masturbation as treatment of premature ejaculation…
  Other people say Masturbation can cause erectile distinction
  Can I get study which support ur statement??

  1. Asante kwa maoni yako Amos. Masturbation sio treatment ya premature ejaculation. Ila ni njia moja wapo ya kucontrol na kumanage hali hii kwa kupunguza hamu. Haitibu premature ejaculation

 4. Naweza kuzuia na kuondoa hali
  hii ya kufika kileleni mapema?

  Kuna mambo mengi ambayo
  unaweza kufanya kabla ya
  kutafuta msaada wa daktari.
  * Kujichua (masturbate) lisaa
  limoja au mawili kabla ya
  kufanya ngono

  hapo sijaelewa vizuri@Daktari Mkononi

 5. Nawapongeza sana daktarimkononi kwa ubunifu mkubwa mlioufanya.Kama mhenga wa sekta ya utabibu, nafarijika sana na hili.
  Baada ya kusoma baadhi ya post zenu ikiwemo hii, ningependa kuwashauri kwamba ni vyema mkaweka References, ili tuweze kusoma zaidi na kupima kama post zenu zinatoa taarifa sahihi.

  Sitilii shaka uwezo wenu, ila katika post hii, nadhani kuna baadhi ya vitu havina uthibitisho wa kisayansi, hilo limenipelekea kuhoji authenticity ya taarifa mnazozileta.

  Nawatakia kazi njema!

 6. Nawapongeza sanaa daktarimkononi kwa ubunifu mkubwa mlioufanya.Kama mhenga wa sekta ya utabibu, nafarijika sana na hili.
  Baada ya kusoma baadhi ya post zenu ikiwemo hii, ningependa kuwashauri kwamba ni vyema mkaweka References, ili tuweze kusoma zaidi na kupima kama post zenu zinatoa taarifa sahihi.

  Sitilii shaka uwezo wenu, ila katika post hii, nadhani kuna baadhi ya vitu havina uthibitisho wa kisayansi, hilo limenipelekea kuhoji authenticity ya taarifa mnazozileta.

  Nawatakia kazi njema!

 7. Literature nyingi zinabainisha kuwa kujichua (masturbation) ni moja kati ya sababu zinazopelekea kulegeza mishipa ya uume na kupelekea kushindwa kusimama kwa uume. Je, Hamuoni kwamba ku recommend masturbation kama njia ya kutibu kumwaga mapema ni kusababisha tatizo kubwa zaidi (la uumekushindwa kusimama) kwa wasomaji wenu??

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show