Muingiliano wa maziwa na dawa.


Utendaji kazi wa dawa unategemea kiwango cha dawa kinachofika katika eneo lengwa kwaajili ya tiba stahiki(affected area). Kuna njia mbalimbali zinazotumika katika mchakato mzima wa kuweka dawa katika mwili wa binadamu, njia hizo ni:

 • Kuchoma sindano.
 • Njia ya hewa.
 • Kupaka katika ngozi.
 • Kunywa/kumeza(vidonge au dawa zilizo katika mfumo wa kimiminika).

Njia ya kumeza/kunywa ni njia ambayo dawa zinaingizwa mwilini kwa njia ya mdomo, njia hii imezoeleka miongoni mwa watu wengi kwa kuwa ni njia inayotumika pasi na uhitaji wa usimamizi mkubwa kutoka kwa wahudu wa Afya, ni sawa na njia ya kupaka kimtazamo wa mazoea ya matumizi.
Njia hii imekuwa ni njia inayotumika sanjari na nyongeza ya baadhi ya vitu kwa malengo mbalimbali, mfano kuna matumizi ya Asali au Sukari ili kupunguza uchungu wa dawa mara baada ya mtu kumeza/kunywa dawa zake.

Dawa huweza kuwa na muingiliano maalumu na baadhi ya vitu tunavyokula wakati tunameza dawa au vile tunavyokula mara baada ya kumeza dawa, muingiliano huu kwa namna moja au nyingine huweza kuingiliana na utendaji kazi wa dawa na pengine kufanya dawa zishindwe kufanya kazi yake ipasavyo hususa ni vile vyakula au vinywaji vinavyopunguza kiwango cha dawa kinachoingia katika mfumo wa damu kutoka katika utumbo mdogo wa binadamu, hivyo si vyema kuambatanisha tendo la unywaji wa dawa pamoja na chakula au kinywaji chochote ambacho hujaelekezwa na muhudumu wa Afya.

Miongoni mwa vitu vyenye utata katika jamii ni swala la muingiliano uliopo kati ya matumizi ya dawa pamoja na Maziwa.
Ndani ya Maziwa kuna aina ya madini yatambulikanayo kama CALCIUM(Ca), madini haya yanauwezo wa kuingiliana na utendaji kazi wa baadhi ya dawa kama Tetracycline na Ciprofloxacin zilizopo katika kundi la Antibiotics na kupunguza utendaji wake wa kazi, madini haya ya Calcium huifanya dawa ishindwe kuingia katika mfumo wa mzunguko wa damu, mfumo huu ndio unaotumika kusafirisha dawa katika maeneo mbalimbali ya mwili na hatimaye dawa hushindwa kufika eneo husika. Sio maziwa pekee yanayoweza kuingiliana na utendaji kazi wa dawa hizo bali pia kuna baadhi ya vyakula vilivyo na madini mengi, vyakula hivi kama bamia na dagaa huweza pia kuingilia utendaji kazi wa baadhi ya dawa. Utumiapo dawa hizo unashauriwa kutumia maziwa au kula vyakula vyenye maziwa baada ya saa moja au mbili ili kuepuka muingiliano unaoweza kujitokeza.

Kuna baadhi ya dawa kama Mseto na Metranidazole ambazo hufanya kazi vizuri pindi zimezwapo na maziwa, pia kuna dawa kama Amoxicillin ambazwo hazina muingiliano wowote na maziwa.

 1. Kunywa dawa kwa kutumia maji ndio njia iliyozoeleka zaidi, maziwa pia yanaweza kutumika chini ya maelekezo maalumu, hivyo ni vyema ukafata maelekezo ya kumeza dawa kama ulivyoambiwa na muhudumu wa Afya, inapotokea kuna kitu kinakutatiza basi ni vyema ukauliza kwa muhudumu wako wa Afya ufafanuzi zaidi.

3 thoughts on “Muingiliano wa maziwa na dawa.

  1. Mwingiliano kati ya phosphorus na dawa au ugonjwa upo. Ila ni kwa njia nyingine sio kama calcium ilivyoelezewa hapa juu.
   Kuna magonjwa kama matatizo ya figo ambayo husababisha wingi wa madini ya phosphorus mwilini hivyo mtu hashauriwi kutumia soda na vyakula vyenye madini hayo sana. Hivyo basi mwingiliano wa dawa na vyakula ipo kwa njia nyingi sanaa, nikielezea yote hapa siwezi maliza. Kwa hiyo tuwatumie wafamasia vizuri katika vituo vyetu vya afya ili kupata maelekezo mazuri tupewapo dawa tule nini na nini tusitumie kwa dawa husika. Asante.

 1. Asante Dr. Josephat Wanawe kwa somo zuri, naomba kueliimishwa kidogo kuhusu mambo 2

  1. Ktk njia za kuweka dawa mwilini, kuna njia ya hewa, sijaielewa vizuri, ningependa na mfano

  2. Umetaka muda wa masaa 2 au zaidi wa kutumia maziwa au baadhi ya vyakula vinavyosababisha dawa isfanye kazi vizuri, je hakuna muda unaotakiwa kwa mtu asitumie vyakula hivyo kabla hajatumia dawa au sio lazima?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show