Ukubwa wa uume. Una mtazamo gani?

Wanaume wengi duniani huwa na wasiwasi kwamba uume wao ni mdogo. Lakini utafiti unaonyesha kwamba wanaume wengi huwa na uume wa kawaida.

Wanaume wengi hujiwekea akilini kuwa uume mkubwa ni kiashiria cha nguvu, ujasiri, utendaji bora wa mapenzi na kadhalika. Wanaume wa makabila mengine wamejaribu kuongeza urefu wa uume wao kwa kurefusha uume tangu umri mdogo kwa kufungia uzito chini yake na wengine hata kuruhusu nyoka ang’ate uume wao.

Kujisikia sio mwanaume kamili kunaweza kuharibu maisha ya mwanaume na kujiamini katika jamii. Baadhi ya makampuni kote ulimwenguni wametumia wasiwasi huu kuuza “vidonge vya kuongeza uume” na bidhaa nyingine za kupanua uume ambazo zinaahidi “kuongeza urefu na ukubwa” kitu ambacho hakijahakikishwa kufanya kazi.

Kupima uume wako.

Hofu na wasiwasi kuhusu ukubwa wa uume huweza pia kutokea baada ya kudharauliwa kutoka kwa watu wengine wakati wa ujana au kufuata maneno kutoka kwa mpenzi.
Hata hivyo, mara nyingi wanaume wana maoni mabaya juu ya uume wao. Unapoangalia chini kwenye uume wako, huonekana kuwa mfupi zaidi kuliko ilivyo kweli. Kuona uume wako kama watu wengine, tumia kioo kirefu. Uume huonekana mkubwa na mrefu kuliko unapoonekana kutoka kwa juu.

Kwa hatua fulani, wavulana wengi huchukua ruler au futi kamba (tape measure) ili kupima urefu wa uume, ni sawa kufanya hivi ila ili kupata kipimo sahihi, fanya hivyo wakati umesimamisha uume, ukianzia kwenye ncha ya juu mpaka chini mwisho.

Uume wa ukubwa gani ni wastani?

Kulingana na utafiti wa 2015 wa wanaume zaidi ya 15,000, vipimo vya kawaida kwa uume wa watu wazima ni:
* urefu: 13.12cm (5.16 inches) wakati uume umesimama

Wanawake wanamtazamo gani juu ya ukubwa wa uume?

Ukiacha kuwa wanaume wengi huwa na uume wa kawaida, wengi bado hawafurahii, wangependa kuongeza ukubwa. Utafiti wa wanaume na wanawake zaidi ya 50,000 umebaini kuwa 45% ya wanaume wangependa kuongeza uume. Asilimia kubwa ya wanawake (85%) wamesema kuwa wameridhika na ukubwa wa uume wa wapenzi wao. Suala la kuvutia kwa wanawake ni ngumu kuelewa. Hata hivyo, tafiti nyingi zinaonyesha kuwa ukubwa wa uume sio kipaumbele kwa wanawake kuliko masuala kama vile tabia ya mwanaume. Linapokuja suala la ngono, wanawake wanavutiwa zaidi na wewe kama unamuonesha mapenzi, upole na unavowasaidia kwa mahitaji yao na sio ukubwa wa uume.

6 thoughts on “Ukubwa wa uume. Una mtazamo gani?

 1. Asantee kwa elimu hii,
  Lakini pia napenda kuongezea kuwa kuna baadhi ya dawa zinazotumika kuongeza urefu wa uume huwa na madhara iwapo zkitumiwa kwa muda mrefu na zikitumiwa kwa ziada yaani overdosage.

 2. Mada nzuri sana
  Natamani ingewafkia wanaume wote maana wengi wamejkutq wakipoteza pesa na muda wao kuhangaikia
  Wimbi kubwa la matapeli lmeibukq kutumia mwanyq huu

 3. Asante sana kwa makala hii, ningependa kuongezea jambo kuwa hizi dawa za kuongeza urefu wa uume huwa zinafanya tissues za kwenye uume (erectile tissues) kuvutika kiasi kinachofanya kutosimama kwa uume sawasawa kama ilivyokua awali.

 4. binafsi sioni kama ukubwa wa uume unachangia kufurahia tendo, tendo linashamiri raha yake wakati wa romance na wanaume wengi tuko wavivu wa kufanya romance kwa muda wa kutosha tukiamini ukubwa wa umbile utasaidia

 5. binafsi sioni kama ukubwa wa uume unachangia kufurahia tendo, tendo linashamiri raha yake wakati wa romance na wanaume wengi tuko wavivu wa kufanya romance kwa muda wa kutosha tukiamini ukubwa wa umbile utasaidia

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show