Je meno yangu yanaweza kuwa meupe?..

Je meno yangu yanaweza kuwa meupe? limekuwa ni swali la watu wengi walio na meno yaliyobadilika rangi na kuwa ya kahawia (Brown discolouration).

Kitaalamu hali ya meno kuwa na  rangi hii huitwa dental flourosis,  tatizo hili ni la moja kwa moja na husababishwa na kiwango kikubwa cha madini ya floridi kwenye meno katika kipindi cha utengenezwaji wa meno mwilini kati ya umri wa mwaka 1 mpaka miaka 4 ya mtoto.Mtoto akiisha fikia umri wa miaka 8 na kuendelea tayari anakua hayupo tena katika hatari ya kupata tatizo hili hata kama atatumia maji yenye kiwango kikubwa cha madini ya fuloridi.

Meno ya rangi hii ya kahawia huonekana sana kwa jamii ya watu waishio maeneo ambayo kuna kiwango kikubwa sana cha madini ya fuloridi katika maji wanayokunywa au hata chakula wanachokula.  Kama madini mengine madini ya floridi yanatakiwa kwa kiwango kidogo tu mwilini na kinapozidi huleta matatizo katika mwili, na moja ya ishara ya kwanza ya matatizo ni kuwa na meno ya kahawia.

Matibabu ya dental flourosis..

Matibabu haya huwa yana mtazamio mkubwa katika kuleta muonekano mzuri wa meno ya mgonjwa. Hivo ni vizuri mgonjwa akashauriana na daktari wake ipi ni njia nzuri zaidi kwake kufanya meno yake kuwa meupe. Matibabu haya hutegemea  ukubwa wa tatizo, yaani ni kwa kiwango gani meno yamebadilika rangi. Aina za matibabu yanayoweza kufanyika ni kama yafuatayo;

 • Tooth whitening(intercoronal bleaching): Njia hii inatumiwa na kuleta matokeo mazuri kwa meno ambayo yameathiriwa kwa kiwango kidogo na tatizo hili.Hapa kemikali maalumu huwekwa ndani ya jino kitaalamu na kulisafisha kisha meno yanakuwa meupe.
 • Veneering : Hii inahusisha kuondoa kidogo sehemu ya juu ya jino na kulijaza au kuziba sehemu hiyo na material maalumu(composite)  yenye rangi nyeupe.
matokeo mazuri baaya ya kufanya veneering
 • Crowning(kuvalisha vikofia juu ya meno):Njia hii inahusisha kuvalisha kofia maalumu crowns ili kuficha ile rangi isionekane.Hii nayo huleta matokeo mazuri sana.

Ifahamike kuwa matibabu haya yanategemeana na ushauri na majadiliano kati ya mgonjwa na daktari wake.Pia kwa kiasi Fulani huwa yana gharama kidogo hivo ni vizuri mtu akajiandaa kifedha kabla ya kuamua kufanya haya matibabu Kujua jinsi ya kuepuka tatizo hili au kuzuia tafadhali endelea kuungana nasi hapahapa kupitia daktari mkononi tutakueleza kwa undani.

 

14 thoughts on “Je meno yangu yanaweza kuwa meupe?..

 1. Shukrani Dr. Charles Ibassoh kwa elimu ya meno, ningependa kufahamu machache yafuatayo;

  1. Njia ya Veneering, je ni material gani hasa yanayotumika yaani yanaitwaje na yametengenezwa kwa kutumia nini?

  2. Je material hayo hayana madhara yoyote au kupunguza uimara wa jino?

  3. Njia ya Crowning, hivyo vikofia havina madhara kwa fizi?

  4. Pia hivyo vikofia ukiishavivalisha, unaweza, kuruhusiwa kuwa unavitoa na kuvirejesha au mpaka hospitali tena?

  5. Mwisho, je ukiweka vikofia unayetumia meno yako kwa kula huku umevivaa au wakati wa kula unavivua?

  1. Asante Charles kwa maswali mazuri,kuhusu veneering ina mambo mengi kidogo ila material inayotumika mara nyingi inaitwa composite,na imeonesha kutokuwa na madhara yoyote kwa watumiaji(biocompartible).

   Pia hivo vikofia(crowns) vinavalishwa hosptali na kuunganishwa moja kwa moja na jino hivo hauhitaji kuvivua na kuvaa ukishawekewa ndo basi vinakaa hapohapo,ingawa unashauriwa kutunza vizur meno hasa ukiwa umewekewa crowns ili kuepuka uhitaji wa kuwekewa nyingine.

   Karibu sana daktari mkononi endelea kushirikiana na sisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show