Nitajuaje mtoto wangu anaonewa? (Bullying)

Kuonewa ni jambo linaloumiza sana watoto na kusumbua akili wazazi. Si jambo la kupuuzia kwa kuwa, mbali na kumtesa mtoto kimwili na kiakili, huweza pia kuvuruga mfumo wake wa hisia kwa muda mrefu, hata kufika ukubwani. Lakini pia tunafahamu kuwa sehemu ya maisha ya ukuaji wa mtoto ni kupitia changamoto za kuumizwa au kuaibika, na jinsi mtoto anavyokabiliana na hali hizi huchangia kwa kiasi kikubwa kujenga ujuzi wake wa kimaisha.

Je, dalili za kuonewa ni zipi? Wakati gani utani hubadilika na kuwa uonevu? 

– Kunapokuwa na tofauti ya nguvu. Mara nyingi uonevu hufanywa na mtu aliye katika nafasi ya nguvu, aidha kimamlaka au mwenye ushawishi zaidi, au hata mwenye nguvu zaidi za kimwili.

– Kunapokuwa na lengo la kudhuru. Uonevu huweza kuwa na lengo la kuleta madhara ya kimwili, maneno, kutishia, kusambaza uongo au kumtenga mtoto katika kundi fulani.

– Ikiwa inajirudiarudia. Uonevu ni mchakato unaojirudiarudia mara kwa mara na kwa mtoto huyohuyo.

– Kunapokuwa na madhara. Yaweza kuwa ya kimwili, kiakili au katika uhusiano wake kwenye jamii.

Jinsi ya kutatua tatizo la uonevu kwa mtoto

– Kamwe usianze kwa kuonesha hisia kali za hasira au mshangao na kuapa kwenda shuleni mara moja au kuongea na wazazi wa mtoto mwonevu. Kudhibiti hisia zako humpa mtoto nafasi ya kuwa muwazi zaidi

– Kabla hujatoa ushauri, kusanya taarifa kamili za tukio zima. Uliza maswali kama “Nani alikuepo?”, “Nini kilitokea?”, “Nini kilisemwa?”, “Ulifanya nini?”, “Ulijisikiaje?”, “Je, kulikuwa na watu wengine?”, “Wengine walikuwa wanafanya nini wakati unaonewa?”na kadhalika. Hii itasaidia kukupa picha ya kilichotokea. Lakini usimkatishe tamaa mtoto kwa kumwambia papo hapo, “Ah hio haina maana.”

Waweza kumshauri yafuatayo:

– Ajiamini anapokabiliwa na mtu mwonevu.

– Atafute marafiki wanaoweza kumsaidia wakati akiwa anaonewa. Pia humsaidia asijihisi mpweke.

– Ajihusishe zaidi na mambo anayopenda kufanya. Hii humsaidia kuhamisha mawazo na kumfanya asijali sana kama ameonewa.

– Kama hali ni mbaya, Waweza kumtafutia mtu mzima atakayekuwa anamwangalia kwa ukaribu mfano mwalimu wake.

– Fuatilia maendeleo ya matukio haya ili kujua kama yanapungua, yanaendelea au yanazidi.

– Muandae mtoto kwa kuongea nae na kumweleza kuhusu uonevu hata kama haijatokea bado.

Mtoto anapolalamika anaonewa shuleni au sehemu nyingine, usipuuzie wala kuchukulia masihara. Msikilize, mpe ushirikiano na ingilia kati panapohitajika. Lakini si vyema kuwajengea akilini kuwa kila hali hasi maishani ni uonevu.

10 thoughts on “Nitajuaje mtoto wangu anaonewa? (Bullying)

  1. Ni kweli wazazi wengi hawajui kama watoto wao wanaonewa huko shuleni hii inaharibu ukuaji wa mtoto kisaikolojia,asante sana dokta kwa maelezo mazuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show