Ugonjwa wa Matezi ya Koo (Tonsillitis)

Matezi ya koo ni kitu cha muhimu katika ulinzi wa mwili hasa kwa watoto kwani hufanya kazi kama ya chujio kuzuia virusi na bakteria wanaoingia mwilini kupitia njia ya pua na mdomo

Wadudu hawa wanapoizidi nguvu tezi hizi ambazo zipo mbili,kulia na kushoto mwishoni mwa kinywa husababisha dalili kuu mbalimbali kama zifuatazo:-

1.Maambukizi ya koo(sore throat)
2.Mafua na pua kuziba Mara kwa mara
3.Homa (hii huambatana na wadudu aina ya bakteria zaidi kuliko virusi)
4.Kukoroma na mtoto kupumulia mdomo,hii hutokana na kuzibwa kwa njia ya hewa kama matezi yamekuwa makubwa sana hasa wakati wa kulala usiku
5.Kupata shida kumeza chakula n.k

Nini cha kufanya
Kwanza ni kuwahi kwenda kituo karibu cha afya kama ikiwezekana ukaenda clinic ya magonjwa ya Pua,Mdomo na Koo (ENT) itapendeza zaidi

Huko utafanyiwa uchunguzi wa kinywa kuona kama kweli matezi yamevimba ndipo utafanyiwa vipimo kujua wadudu walioleta ugonjwa kama ni bakteria au virusi na kupewa dawa husika

Kama ni bakteria dawa zipo(antibiotic) husaidia kutibu pia dawa za maumivu,za kuzibua pua na Mara nyingine hata za allergy hutumika kumpa unafuu mtoto

Kwa virusi mara nyingi huisha yenyewe bila dawa ila mzazi/mlezi anaweza hakikisha mtoto
1.Anapumzika vya kutosha
2.Anakunywa vinjwaji kama maji yaliyopoa/vuguvugu
3.Anakula vyakula vilaini
Ili kumsaidia kupona kwa haraka na kupunguza maumivu kwenye koo kwa kipindi ambacho Cha ugonjwa huu

Matezi ya koo yanaweza kutolewa pia kwa upasuaji mdogo kulingana na jinsi daktari atakavyoona dalili za mtoto na kushauriana na mzazi/mlezi

4 thoughts on “Ugonjwa wa Matezi ya Koo (Tonsillitis)

  1. Asante dokta kwa maelezo mazuri,,je ni kweli kula vyakula vya baridi vinasababisha kupa tonsillitis? maana enzi ya utoto tulikuwa tunakatazwa kula barafu kuogopa hyo kitu je kuna ukweli wowote?!

    1. Asante kwa swali lako Sarah….hakuna uhusiano wowote baina ya vinywaji vya baridi na tonsillitis.Njia kuu ugonjwa huu husambaa ni kwa kushikana(contact) hapa ndipo wadudu watatoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine
      Mfano.kushare glass moja ya maji,kumshika mgonjwa mkono baada ya kupiga chafya na kadhalika

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show