Ufahamu ugonjwa wa moyo kwa watoto uitwao Rhumatiki ya moyo(Rheumatic heart disease)

Huu ugonjwa huwaathiri zaidi watoto wenye umri kuanzia miaka 5-15, kuliko watu wazima.. na mara nyingi mtoto huzaliwa nao. Watu weusi huathiriwa zaidi kuliko wazungu na huwapata wanaume au wasichana kwa usawa

Mara nyingi husababishwa na bacteria waitwao GABHS na hufwata baada ya kipindi cha homa ya rhumatiki… Bacteria hao huamsha kinga ya mwili na kuharibu valve za moyo kwa kukaza hasa ya upande wa kushoto wa moyo…. hii husababisha moyo usisukume damu vizuri kwenda sehemu husika.

Vichechezo vya ugonjwa huu ni kama
. Maambukizi ya njia ya upumuaji ya mara kwa mara
. Historia ya ugonjwa huo kwenye familia
. Hali ya chini ya maisha
. Kuishi sehemu ya watu wengi(msongamano)

Viashiria vya ugonjwa huu ni,
Uthibitisho wa huu ugonjwa ni mtu akiwa
1. Ashiria 2 kii na 1 ndogo au
2. Ashiria 2 ndogo na uthibitisho wa kuambukizwa na bacteria hao.

Ashiria kuu- maambukizi ya viungo vya, maambukizi ya misuli ya moyo, vinundu chini ya ngozi, alama nyekundu kwenye ngozi na harakati za viungo vya mwili zisizo na mpangilio

Ashiria ndogo- maumivu ya viungo , homa na mabadiliko ya moyo kwenye mashine

Dalili za ugonjwa
1. Maumivu ya viungoni au kifua
2. Homa kali
3. Uchovu au kushindwa kufanya kazi
4. Moyo kuenda mbio
5. Alama nyekundu kwenya ngozi

Nini cha kufanya endapo unahisi mtoto wako ana ugonjwa huu
Mkimbize mtoto kwenye kituo cha afya kwa vipimo ma matibabu zaidi.

4 thoughts on “Ufahamu ugonjwa wa moyo kwa watoto uitwao Rhumatiki ya moyo(Rheumatic heart disease)

  1. Shukrani Dr. Maureen Rishya kwa maelezo yako.

    1. Kwanini ugonjwa huu unawaathiri weusi zaidi ya wazungu?

    2. Je hali ya chini na kuishi kwenye msongamano kunachochoea vipi mtu kuupata huu ugonjwa?

    1. 1. Nchi za watu weusi mara nyingi zina tatizo la umasikini unaofanya watu waishi katika misongamano ambamo ni rahisi kwa bacteria huyu kusambazwa na pia hata tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu kwa kupata chanjo hazijaendelea sana kwenye nchi za hali ya chini.

      2. Bacteria huyu huathiri sana ngozi na mfumo wa upumuaji(hewa) na kusababisha maambukizi… na huwa huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwa mwingine kwa kukohoa au kugusana ambapo ni rahisi zaidi kwenye sehemu ya msongamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show