Vidonda vya kujirudia mara kwa mara mdomoni(apthous stomatitis)

Kuna watu hupata vidonda mdomoni mara kwa mara na hakumbuki alivipataje,yawezekana una tatizo la vidonda vya kujirudia ambalo kitaalamu  linajulikana kama reccurent apthous stomatitis.Vidonda hivi vinawapata watu wote hasa wasomi na watu wenye maisha ya juu kiuchumi.

Vidonda hivi hutokea maeneo yote ya ndani ya mdomo na sehemu ya ndani ya mashavu.Watu wengi wanapata  kidonda kimoja tu wengine viwili na kuendelea vya ukubwa tofauti  kuanzia chini ya sentimita moja na kuendelea.Baadhi ya watu hupata maumivu makali wakashindwa kuvumilia wengine huweza kuyavumilia.Vidonda hivi vinaweza kusababisha mtu kushindwa kutafuna chakula vizuri hata kushindwa kuongea hivo vinahitaji uangalizi pale vinapozidi.

Sababu ya kutokea vidonda hivi haijulikani moja kwa moja lakini kuna baadhi ya vitu huwa vinahusianishwa na vidonda hivi kama:

 • Msongo wa mawazo na hitilafu kwenye homoni za mwili.
 • Hitilafu kwenye mfumo wa kinga ya mwili.
 • Kujiumiza na meno au vitu vingine.
 • Ukosefu wa baadhi ya vitamini kama vitamin B12,Folic acid na madini chuma mwilini.
 • Maambukizi yatokanayo na bakteria au virusi aina ya herpes zoster.
 • Wengine huwa ni vya kurithi yaani kama mtu ana historia ya vidonda hivi kwenye familia yake.
 • Madhara yatokanayo na kula vyakula(allergy) Fulani kwa baadhi ya watu kama vyakula vyenye kimea,jamii ya karanga na chokleti.

Dalili za vidonda hivi

 • Hisia ya kuungua na muwasho kidogo kwenye eneo husika kabla kidonda hakijatokea
 • Kidonda hutokea na huwa na maumivu makali hasa siku 4 za mwanzo

Vidonda hivi huwa vinapona vyenyewe baada ya siku 7 mpaka 10 kwa mtu mwenye afya nzuri.Ikizidi hapo onana na daktari wa meno kupata msaada wa kitaalamu na kujiridhisha kama ndo vyenyewe, pia unashauriwa kufanya yafuatayo.

 • Kuepuka au kupunguza msongo wa mawazo
 • Kula mlo kamili wenye virutubisho vyote
 • Kuepuka kutumia vyakula ambavo vinakuletea madhara kama unavifahamu.
 • kusukutua kwa maji ya uvuguvugu yenye chumvi kiasi angalau mara mbili mpka nne kwa siku
 • weka kipande cha barafu kwenye kidonda hii hupunguza maumivu
 • Tumia dawa za kutuliza maumivu kama maumivu ni makali
 • Ukionana na daktari wa kinywa na meno anaweza kukupatia dawa za kupaka za kupunguza maumivu, dawa za kusukutua na kuua vijidudu kama kuna maambukizi .

 

 

 

12 thoughts on “Vidonda vya kujirudia mara kwa mara mdomoni(apthous stomatitis)

 1. The causes is not completely understood, but involves a T cell-mediated immune response triggered by a variety of factors. Different individuals have different triggers, which may include nutritional deficiencies, local trauma, stress, hormonal influences, allergies, or genetic predisposition.
  Diagnosis
  By hx of a pt and clinical examination
  Treatment
  No need of antibiotics in early stages you can give pain killers, oral and advice to eat balance diet plus oral personal hygiene.

 2. Daktari kuna kipindi hata kupiga mswaki ilikuwa shida kuweka maji ya baridi mdomoni, Lakini Leo umenifumbua macho na nimepanua uelewa nilikuwa na Mawazo sana kipindi hicho😀

  1. karibu sana Bertha vyakula vyenye hayo madini viko vingi sana,nitakutajia kwa uchache,lakini cha msingi ni kuhakikisha kuwa una kula mlo kamili kila siku.
   B12..bidhaa za maziwa,nyama nyeupe kama kuku na samaki.
   folic acid..mboga za majani kama chainizi,matunda jamii ya machungwa,limao
   Iron..Nyama,maini,nafasa zisizokobolewa na maharagwe na soya.

 3. Asante kwa kutupatia njia ya kujihudumia nyumbani,sikuwahi kujua maji ya chumvi yanaweza kuwa na msaada,mimi ni muhanga mkubwa wa hivi vidonda.

  1. karibu sana Bertha vyakula vyenye hayo madini viko vingi sana,nitakutajia kwa uchache,lakini cha msingi ni kuhakikisha kuwa una kula mlo kamili kila siku.
   B12..bidhaa za maziwa,nyama nyeupe kama kuku na samaki.
   folic acid..mboga za majani kama chainizi,matunda jamii ya machungwa,limao
   Iron..Nyama,maini,nafasa zisizokobolewa na maharagwe na soya.

 4. Thanks a lot for this education I see you’re bringing awareness to us who are lazy on following up health issues but I advise you to come up with an application either on google play store or else I am sure that way you will reach more people and easy access on follow up your publishes.
  Thanks a lot God bless you

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show