Zijue sababu saba (7) ambazo zinaweza pelekea mtoto kuzaliwa na tatizo la moyo (congenital heart diseases).

Magonjwa mengi ya moyo ambayo mtoto anaweza zaliwa nayo huwa hakuna sababu ya moja kwa moja ila yamehusishwa na sababu mbalimbali za kimazingira na vinasaba(genetics).

Moja ya sababu hizo ni;
1. Unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.
2. Maambukizi ya virusi aina ya rubela wakati wa ujauzito hasa wiki 13 za kwanza kipindi cha kwanza cha ujauzito. Ni vema kupata chanjo ya rubela kabla ya ujauzito ili kupunguza uwezekano wa mtoto kuzaliwa na ugonjwa na moyo.
3. Utumiaji wa baadhi ya madawa ambayo si salama wakati wa ujauzito kama vile Phenytoin na Lithium.
4. Uvutaji wa sigara na utumiaji wa madawa ya kulevya wakati wa ujauzito.
5. Vinasaba(genetics), wakati mwingine hutokea kwa familia fulani ambazo zinaweza kuwa na viashiria vya magonjwa ya kurithi kama vile ugonjwa wa udumavu (Down syndrome).
6. Kisukari kisichodhibitiwa vizuri wakati wa ujauzito. Hiki ni kile kisukari ambacho mtu alikua nacho hata kabla ya ujauzito na si kile ambacho mama mjamzito anakipata kwa sababu ya ujauzito (gestational diabetes).
7.Kutopata lishe sahihi wakati wa ujauzito.

Sababu nyingi zinaepukika, hivyo ni vema kuchukua hatua mapema kabla na wakati wa ujauzito ili kujiweka mbali na hatari ya kupata mtoto mwenye ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao.

8 thoughts on “Zijue sababu saba (7) ambazo zinaweza pelekea mtoto kuzaliwa na tatizo la moyo (congenital heart diseases).

 1. Asante dokta kwa elimu mimi nna swali,je wale watu wa vijijini ambao wengi wao wanakula vizur na hawana tabia kama za uvutaji wa sigara wala hawajibweteki wakati wa ujauzito na bado wengine wana pata watoto wenye matatizo ya moyo sababu huwa ni nini hasa?!

  1. Nashukuru kwa swali zuri, Salama Tendwa.
   Kama nilivyosema hapo awali kuwa mara nyingi magonjwa hayana sababu ya moja kwa moja ingawa watu wengi hurithi kupitia vinasaba kutoka kwa wazazi wao au kizazi cha nyuma.

  1. Nashukuru kwa swali zuri ndugu, Dorothea.
   Kwa sababu unakunywa pombe siyo lazima mtoto wako atazaliwa na ugonjwa wa moyo lakini kwa kutumia pombe wakati wa ujauzito unakua katika hatari ya kupata mtoto mwenye ugonjwa wa moyo.
   Kuhusu kuacha pombe, hili ni swala la wewe mwenyewe kwa dhamira yako kutaka kuacha kutumia pombe, unaweza jiongoza wewe binafsi au ukakutana na wataalamu ambao watakushauri jinsi ya kuacha kutumia pombe (through motivational interview technique)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show