Maambukizi katika mfumo wa juu wa hewa

Haya ni maambukizi ambayo huwaathiri sana watoto na mara nyingi husababishwa na virusi (viruses). Maambukizi haya huwapata mara kwa mara zaidi watoto kuliko watu wazima kwasababu kinga ya mwili ya watoto bado haijajengeka vizuri na bado si imara ili kuweza kupambana na virusi hivi vinavyo sababisha maambukizi haya. Maambukizi haya ni kama: mafua na matezi ya koo, lakini pia maambukizi haya huweza kufika mpaka kwa ndani ya maskio.

Dalili ambazo mwathirika anaweza kuwa nazo ni pamoja na:

 • Homa.
 • Kutokwa sana na makamasi na pua kuziba kwasababu ya makamasi.
 • Pia hasa kwa watoto mafua yatamfanya awe anapumua, anakula na kulala kwa shida.
 • Kuumwa kichwa
 • Kubadilika kwa sauti na kuwa kama inakwaruza (hoarse voice).
 • Koo kuuma pamoja na kukohoa.
 • Kupiga sana chafya.
 • Kuhisi uchovu na udhaifu.

Kwasababu maambukizi haya husababishwa na virusi, basi huwa yanaisha yenyewe baada ya muda fulani na mwathirika kupona kabisa. Na hii ni baada ya mwili kujenga kinga ya kutosha kupambana na kuviua virusi hivyo.

Lakini pia maambukizi haya yanaweza yasiishe tuh yenyewe, bali yakazidi na kusababisha madhara makubwa kwa mwathirika. Zifuatazo ni dalili za hatari ambazo kama mwathirika akizipata ni muhimu kumwahisha hospitali au kituo cha afya kilicho karibu kwaajili ya matibabu:

 • Upungufu wa pumzi.
 • Kupumua kwa haraka.
 • Kumeza kwa shida au kushindwa kabisa kumeza.
 • Kuwa mchovu sana na mdhaifu sana.
 • Kupatwa na kizunguzungu au kupoteza fahamu.

Pia ni vigumu kuzuia maambukizi haya kwani virusi wengi ambao huweza kusababisha maambukizi haya wapo kwenye hewa ambayo tuna pumua.

 

 

4 thoughts on “Maambukizi katika mfumo wa juu wa hewa

 1. Shukran kwa elimu ya afya hasa kwa katika mfumo wa hewa kwani ni watoto wengi hupoteza maisha kutokana na magonjwa hayo.
  Kazi njema.

 2. Shukrani sana Dr Johnson, kiufupi daktari Mkononi mmekua na faida kubwa sana kwangu na familia yangu; ninawapongeza kwa hilo.
  Swali langu ni kwamba umeelezea kuhusu magonjwa ya mfumo wa juu wa hewa, sasa ugonjwa huo unafikaje kwenye masikio na ni dalili gani nikipata ndo nitajua umefika kwenye masikio

  1. Sikio la binadamu limegawanyika katika sehemu tatu, sikio la nje linalo onekana, sikio la kati na sikio la ndani, sasa sikio la kati limeunganishwa na mfumo wa juu wa hewa kupitia njiaa iitwayo neli ya koromeo (eustachian tube). Hivyo mtu akipata maambukizi bakteria huweza kusaamba mpaka kufika kwenye sikio kupitia njia hii. Dalili ambazo unaweza kuzipata kutokana na maambukizi haya kufika sikioni ni pamoja na; kupatwa na maumivu ya skio, kutokuskia vizuri na homa. Karibu tena na asante kwa swali lako zuri Veronica.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show