Njia ya hewa ya watoto.

Njia ya hewa ni sehemu muhimu sana katika uhai wa mwanadamu. Matatizo ya upumuaji huchangia kwa asilimia kubwa katika vifo vya watoto chini ya miaka mitano barani Africa. Pia njia ya hewa ya watoto inatofautiana na ya watu wazima katika maumbile yake. Njia ya hewa ndiyo hatua ya Kwanza katika kuokoa maisha ya mtu na hii inasababisha tuwe na tahadhari ya pekee katika swala hili.

Sifa za njia za watoto kulinganisha na watu wazima

  • ni nyembamba na hivyo huathirika kwa urahisi zaidi na makamasi(mafua), uvimbe katika kuta za njia ya hewa utokanao na maradhi mbalimbali (inflamation), na kupaliwa na vitu mbalimbali vinavyoweza kuziba njia hiyo.
  • taya ndogo
  • wana kichwa kikubwa na hivyo kufanya shingo kuinama kwa mbele na kuziba njia ya hewa hasa anapolala chali.
  • ulimi mkubwa (huweza kuziba njia ya hewa mtoto anapopoteza fahamu).
  • njia ya hewa imekunjika kwenda mbele zaidi kuliko ya mtu mzima
  • epiglotis (kinyama kinachofunika njia ya hewa na kuzuia chakula kisiingie kwenye mfumo wa upumuaji) nikirefu zaidi na kigumu
  • koromeo fupi ina hatari zaidi ya kujikunja kuzuia upumuaji

Nini waweza kufanya kumsaidia mtoto wako kupumua pindi anapopata shida ya kupumua.

  • hakikisha hamna kitu kilichoziba njia ya hewa. hii inaweza kuwa chochote kile katika mazingira ambacho watoto hupenda kuchezea m.f sarafu(coin), mbegu za nafaka (maharage, kunde), nk
  • mfute kwa kitambaa kisafi kama ana matemate (secretions) kinywani au puani mengi isivyo kawaida.
  • kunja kipande cha nguo na weka nyuma ya mabega ya mtoto. Hii itasaidia kupunguza shingo kukunja na hivyo kufungua zaidi njia ya hewa.

Waweza kufanya haya kama huduma ya kwanza ili kumsiadia mtoto apumue vizuri lakini hakikisha unampeleka mtoto hospitali ili kupata matibabu na msaada zaidi.

reviewed by Dr. Kilalo Mjema

3 thoughts on “Njia ya hewa ya watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show